Friday 3 February 2017

Rais Magufuli Ateua Mkuu Mpya wa Majeshi


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli, amemteua Luteni Jenerali Venance S. Mabeyo kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania.

Pamoja na kuteuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Luteni Jenerali Venance S. Mabeyo amepandishwa cheo na kuwa Jenerali.


Jenerali Venance S. Mabeyo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jenerali Davis Mwamunyange ambaye amestaafu.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Major Jenerali James M. Mwakibolwa kuwa Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania.

Pamoja na kuteuliwa kuwa Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Major Jenerali James M. Mwakibolwa amepandishwa cheo na kuwa Luteni Jenerali.

Luteni Jenerali James M. Mwakibolwa anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jenerali Venance S. Mabeyo ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania.

Uteuzi huu unaanza mara moja na tarehe ya kuapishwa itatangazwa baadaye.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!