Tuesday, 21 February 2017

MUHIMBILI YAFANYA UPASUAJI MKUBWA WA KWANZA WA WATOTO

Madaktari wakifanya upasuaji wa njia ya matundu madogo kwa mtoto huyo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH). 

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imefanya upasuaji mkubwa kwa njia ya matundu madogo (Laparoscopy Surgery) kwa watoto ambao haujawahi kufanyika hapa nchini.
Upasuaji huu umefanywa na Madaktari Bingwa wa Muhimbili waliobebea katika upasuaji wa watoto kwa kushirikiana na mtaalam kutoka Hospitali ya King Faisal ya nchini Saudia Arabia.
Kwa mujibu wa Daktari Bingwa wa Upasuaji wa watoto wa Hospitali hiyo, Zaitun Bokhary leo umefanyika upasuaji wa nyama iliyojitokeza sehemu ya haja kubwa kwa mtoto pamoja na upasuaji wa kuondoa kifuko cha ziada katika mfuko wa chakula.
Upasuaji huu mkubwa ambao umefanyika leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili hufanyika nchi zilizoendelea hivyo Tanzania ni mara ya kwanza kufanyika na utaleta mageuzi makubwa nchini.
Moja ya faida kubwa ya upasuaji wa aina hii ni mgonjwa kupona haraka na gharama kidogo hutumika wakati wa upasuaji tofauti na upasuaji wa kufungua tumbo.
Upasuaji ambao umeanza leo unahusisha upasuaji wa nyama iliyojitokeza katika sehemu ya haja kubwa kwa watoto, upasuaji wa kushusha kokwa katika korodani, upasuaji wa kushusha utumbo mkubwa na kutengeneza njia ya haja kubwa kwa watoto ambao wamezaliwa bila kuwa na njia ya haja kubwa, upasuaji wa kuondoa mfuko wa ziada kwenye koo kwa watoto na upasuaji kwa watoto wadogo ambao hawana celi mbalimbali na hivyo kushindwa kusukuma choo kwenye utumbo mkubwa.
Kutoka kushoto ni daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk. Zaitun Bokhary, Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto, Profesa Zakaria Habib kutoka Falme za Kiarabu na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto wa Muhimbili, Dk Mbaga wakifanya upasuaji LEO wa njia ya matundu madogo ( Laparoscopy Surgery) wa kuondoa kifuko cha ziada katika mfuko wa chakula kwa mtoto mwenye umri wa miaka 10.
Dk Zaitun wa Muhimbili akizungumza na waandishi wa habari kuhusu upasuaji huo uliofanyika leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!