Tuesday 21 February 2017

Maduka ya wahamiaji yaporwa Afrika Kusini


Wahamiaji wa Afrika na kutoka Asia hukumbwa na ghasia nchini Afrika Kusini
Haki miliki ya pichaAFP
Image captionWahamiaji wa Afrika na kutoka Asia hukumbwa na ghasia nchini Afrika Kusini
Zaidi ya maduka 30 yanayomilikiwa na raia wa kigeni yameporwa sehemu mbili tofauti kwenye mji mkuu wa Afrika Kusini Pretoria.

Uporaji huo ulianzia eneo la Atteridgeville na kusambaa hadi eneo lililokaribu la Lotus Gardens. Hata hivyo polisi walifanikiwa kutuliza hali.
Mkutano wa makasisi wa kanisa katoliki wa nchi za kusini mwa Afrika, umeitaka serikali kudhibiti mipaka. Pia makasisi hao wametaka mashirika ya usalama kutambua ghasia kabla hazijalipuka.
Afrika ina ukosefu wa ajira wa asilimia 25 sababu ambayo imesababisha wageni kulengwa tangu umalizike ubaguzi wa rangi mwaka 1994

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!