Wednesday, 25 January 2017

Umeme wakatika ghafla Tanzania

Afisa wa uchaguzi Tanzania akijaza fomu za uchaguzi kwa kutumia taa ya umeme Oktoba 25, 2015.Haki miliki ya pichaAFP/GETTY
Maeneo yote yaliyounganishwa kwenye mfumo wa taifa wa kusambaza umeme Tanzania asubuhi yameathiriwa na kukatika kwa ghafla kwa umeme.

Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania limesema tatizo hilo limesababishwa na hitilafu katika mtambo wa kupooza na kusambaza umeme eneo la Ubungo, Dar es Salaam.
Umeme ulikatika mwendo wa saa kumi na mbili unusu asubuhi.
Kituo hicho cha Ubungo ni kituo kinachotumiwa kudhibiti na kusambaza umeme mikoa yote ukiondoa mikoa ya Kagera na Kigoma inayopata umeme kutoka nchi jirani ya Uganda.
Kaimu meneja uhusiano wa Tanesco, Leila Muhaji amesema wataalam wanaendelea kushughulikia tatizo hilo.
"Tatizo hili limetokea leo saa 12:32 asubuhi katika mtambo wa kilovolti 220 ambao ni wa kupoozea na kusambaza umeme uliopo Ubungo lakini kwa kuwa wataalam wameshagundua," Muhaji amesema.
Hitilafu hiyo iliathiri pia mitambo ya kusukuma maji katika shirika la maji DAWASCO, mitambo mitatu ya Ruvu juu, Ruvu chini na mtambo wa mtoni na hivyo huduma ya maji pia kukosekana kwani mitambo hiyo kutegemea umeme kufanya kazi.
Evalastin Liyaro ambaye ni kaimu meneja uhusiano wa shirika la maji safi na maji taka Dar-Es-Salaam amesema baadhi ya maeneo yanatarajiwa kukumbwa na uhaba wa maji ama kukosa huduma hiyo kwa muda usiojulikana.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!