Mlonge: Mmea wa maajabu kwenye lishe


KAMA kuna mti wenye faida nyingi za kiafya, basi mlonge unaweza kuwa unaongoza. Baadhi ya wataalam wa tiba asilia wanaeleza kuwa kila eneo la mti huu, kuanzia majani, maua, mbegu, magamba hadi mizizi yake ina virutubisho vya kipekee vyenye faida nyingi za kiafya kwa binadamu.









KAMA kuna mti wenye faida nyingi za kiafya, basi mlonge unaweza kuwa unaongoza. Baadhi ya wataalam wa tiba asilia wanaeleza kuwa kila eneo la mti huu, kuanzia majani, maua, mbegu, magamba hadi mizizi yake ina virutubisho vya kipekee vyenye faida nyingi za kiafya kwa binadamu.
Majani ya mlonge yanaweza kutafunwa mabichi, yaliyochemshwa kama mboga au yaliyokaushwa na kusagwa kuwa unga. Unga wa mlonge unaweza kuhifadhiwa kwa miezi kadhaa bila kupoteza ubora na faida zake za kiafya.
Inadaiwa kuwa majani ya mlonge yana Vitamin A nyingi kuliko karoti, vitamin C nyingi kuliko machungwa na madini ya Potassium nyingi kuliko ndizi mbivu na kwamba protini yake ni bora kuliko maziwa na mayai.
Mlonge pia unadaiwa kuwa na kiasi kikubwa cha madini ya chuma na hivyo una uwezo mkubwa wa kuimarisha mifupa na kusafisha mfumo wa damu mwilini.
Siyo hivyo tu, mti wa mlonge unatibu zaidi ya magonjwa 300 ya aina mbalimbali, yakiwamo sugu kama pumu, kikohozi, kifua kikuu, kisukari, shinikizo la damu na kuongeza kinga ya mwili.
Pia mbegu za mmea huo zinatajwa kuwa na uwezo wa kutibu malaria na kusaidia hamu ya kunywa maji na magome yake yanaweza kusafisha maji.
Kadhalika, mlonge unaweza kutibu harufu mbaya mdomoni.
Magonjwa mengine yanayotibika kwa mbegu hizo ni malaria sugu, pumu, matezi, saratani na maumivu ya mwili huku mafuta ya mbegu hizo yakiwa ni dawa ya kuchua maumivu ya mwili.
Majani ya Mlonge yamepachikwa jina la chakula chenye viwango kwa sababu wanasayansi waligundua yana kiasi cha madini ya Kalisium yanayoweza kupatiakana katika glasi nne za maziwa, kiasi cha vitamini c inayopatikana kwenye machungwa saba, Potasium ya kwenye ndizi mbivu tatu.
Pia unapata kiasi cha madini ya chuma mara nne zaidi ya kiasi kinachopatikana kwenye spinachi, kiasi cha vitamani A mara nne zaidi ya kile kinachopatikana kwenye karoti na kiasi cha protini mara mbili zaidi ya kile kinachopatikana kwenye maziwa.
Ukiwa na mti wa mlonge ni sawa na kuwa na Supermarket kwenye mti.
Unaweza kuweka kijiko kimoja kwenye chakula cha mtoto au chakula cha familia kila siku ili kujipatia virutubisho hivyo.
Kutokana na faida nyingi za mmea huu, unashauriwa uwe na mashina kadhaa ya mmea huu kwa matumizi ya familia.