Tuesday 24 January 2017

Manara wa Simba kumposa Wema Sepetu?

Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Simba Haji Manara ameendelea na kueleza hisia zake za kutofurahishwa na shirikisho la soka Tanzania TFF kwa kile anachokiita kutokuwa makini na upangaji wa ratiba za Ligi bila kubadilibadili ambapo ameandika yafuatayo.


RATIBA TU NI MUHALI,,HAYO MENGINE KWETU SI BAHARI ??* Haji S Manara. Kuna kurogwa na kujiroga, Kuna kufa na kujiua pia kulia na kuliliwa, sisi watanzania hakika tupo katika fungu la pili, fungu la kukosa , fungu mzigo, tunajiroga, tunajiua na tunaliliwa
Hakika hatujui tunataka nini, hatujui malengo yetu lakini kubwa hatujui hata tutokapo wala tuendako, na leo naandika kitu kidogo tu kinachotushindwa kwenye soka letu, RATIBA
Wakati wenzetu wanazungumzia changamoto nzito na kubwa katika maendeleo yao ya mchezo murua zaid duniani wa soka, Watanzania tunahangaika namna ya kupanga ratiba ya mechi zetu za ligi yetu na kombe la shirikisho,
Ratiba inayobadilishwa kama nguo, tena mvaaji mwenyewe ni mbunifu wa mavazi au mwanamitindo ambaye huvaa nguo tano kwa siku, siku za nyuma niliwahi kuwaambia CLOUDS FM kuwa iwapo ratiba ya Ligi kuu nchini haitopanguliwa nitatembea bila shati toka Mtaa Msimbazi hadi zilipo ofisi za TFF.
Nilidhani Kwa kusema vile walau TFF na bodi ya Ligi wataona haya na kuhakikisha ratiba ya Ligi kuu haitabadilishwa tena, kumbe ndio kwanza wakubwa wameweka gundi masikioni, toka wakati ule ratiba ishafumuliwa mara tatu.
Leo hii imebadilishwa tena kwa kisinguzio kile kile eti ratiba za CAF na za ligi zimeingiliana, ninajiuliza iwapo ratiba ya Ligi yetu ni shida kuipanga, vipi kuhusu program nyingine za maendeleo? Itakuwaje kuhusu timu yetu ya taifa juu ya ndoto zetu za mchana wa jua kali? vipi kuhusiana na zile programu hewa za soka la vijana, watoto na wanawake?
Hakika kwetu hayo ni sawa na bahari ya Mediteranean au bahari kuu ya hadithi za Alfu Leila uleila, hatuwezi ratiba tutaweza kwenda AFCON 2019? hatuwezi kupanga ratiba tutaweza kuwa na mipango madhubuti ya kuendeleza mchezo huu ambao yatajwa watu bilioni tatu duniani kote wanaushabikia?
Nimalizie Kwa kuwapa mtihani mwingine TFF na bodi ya Ligi, iwapo Kama ratiba yao ya Ligi kuu na Kombe la shirikisho haitabadilishwa kuanzia sasa hadi mwisho wa msimu, nItamposa mlimbwende Wema Sepetu, na akikubali nitamuoa, akikataa nitatembea na boxer toka nyumbani kwangu hadi TFF..

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!