Monday, 23 January 2017

KESI YA MKE WA BILLIONEA MSUYA YAPIGWA TAREHE NYINGINE

Image result for MKE WA BILIONEA MSUYA
Mahakama ya Hakimu Kisutu imeshindwa kuamuru kesi ya mauaji inayomkabili mke wa marehemu bilionea Erasto Msuya na kuaihirisha tena hadi Februari 6 mwaka huu.


Hayo yametokea leo baada ya wakili wa serikali Kishenyi Mutalemwa kuieleza mahakama kuwa kesi hiyo ingesomwa kwaajili ya kutolewa maamuzi lakini Hakimu Mkazi Mkuu Godfrey Mwambapa anayesikiliza kesi hiyo alisema hawezi kusikiliza kesi hiyo kwasababu kuna barua kutoka kwa ndugu wa Msuya na anasubiri maelekezo.
Hakimu Mwambapa alitakiwa atoe hoja zinazowasilishwa upande wa utetezi pamoja na upande wa mashtaka ambapo wakili John Malya aliomba washtakiwa hao waachiwe huru kwasababu hakuna hati ya mashtaka inayowashikilia washtakiwa hao mahakamani hapo.
Kwa upande wake Wakili wa serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa aliiomba mahakama iwape muda ili waweze kutekeleza amri ya mahakama iliyotolewa Januari 9, 2017.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!