Friday, 16 December 2016

Wananchi waiomba serikali kusaidia kutafuta miili ya watu watano wanaosadikiwa kuzama maji katika ziwa Victoria.

Wananchi wa kijiji cha Kino na Rubili kisiwa cha Mazinga wilaya ya Muleba mkoa wa Kagera wameiomba serikali msaada wa kusaidia kutafuta miili ya watu watano wanaosadikiwa kuzama maji katika ziwa Victoria siku tatu zilizopita baada ya mitumbwi waliyokuwa wakitumia kwenye shughuli za uvuvi wa samaki kuzidiwa na dhoruba ya upepo mkali.



Mmoja wa watu walionusurika kifo kati ya watu sita waliozama maji katika ziwa victoria wakiwa kwenye mitumbwi mitatu tofauti ambaye hakuwa tayari kuzungumza mbele ya kamera huku akiruhusu picha yake itumike bila kuzungumza amesema kuwa ajali hiyo imetokea usiku wa manane majira ya saa tisa na dakika 30 ambapo mvua iliyoambatana na upepo mkali ilitokea ghafla na kuwazidia jambo lililosababisha mitumbwi waliokuwa wakitumia kuzama maji ambapo yeye alijinasua kwenye kifo kwa kushikilia mtumbwi uliokuwa ukizama na kuibuka majini hadi alipookolewa na wavuvi wenzake .
Asubuhi yake wananchi walijikusanya na kwenda kutafuta miili ya watu watano usiku na mchana bila mafanikio huku wakichangishana fedha za kununua mafuta kwa ajili ya boti na wengine wakitumia mitumbwi ya kasia hali iliyowaladhimu kuomba msaada wa serikali.
Hiyo ni kamati ya ulinzi na usalama ambayo imelazimika kwenda kwenye eneo la tukio katika kisiwa cha Mazinga wakitumia boti maalum pamoja na mambo mengine serikali imetoa msaada wa mafuta ya boti kwa ajili ya kutafuta miili ya watu watano wanaosadikiwa kuzama maji katika ziwa Victoria.

ITV.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!