Friday 9 December 2016

Kutoka Uwanja wa Uhuru Dar, Sherehe za Miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania

1

UHURU: Rais Magufuli amemaliza kuzungumza na Taifa, amesalimiana viongozi mbalimbali wa serikali na siasa na kuondoka kwenye Uwanja vya Uhuru jijini Dar, Sherehe za 55 za Uhuru wa zimefungwa rasmi.

JPM: Rais Magufuli amesema mwaka huu ndiyo wa mwisho kuadhimisha sherehe za uhuru jijini Dar, kuanzia mwakani sherehe hizo zitaadhimishwa Makao Makuu ya nchi mjini Dodoma.
JPM: Amesema hakutakuwa na chakula wala Dhifa ya Taifa kama miaka mingine baada ya Sherehe za Maadhimisho ya 55 ya Uhuru yaliyofanyika leo Uwanja wa Uhuru, Dar.
JPM: Rais Magufuli amesema mwaka jana alikataza kuadhimisha sherehe za uhuru kwa kuwa ilikuw ni takribani mwezi mmoja tu tangu aapishwe, hakuwa ameteua Baraza la Mawaziri pamoja na watendaji wengine, licha hivyo gaharama za kufanikisha sherehe hizo zilikuwa kubwa kiasi cha Tsh Bilioni 4 wakati serikali haikuwa na pesa.
“Mambo mengi yalitakiwa kufanyika ikiwemo kulipa posho pamoja na chakula cha wageni, Je, chakula hicho wanakula wananchi wote? Jibu ni hapana, ndiyo maana nikaona nizifute. Amesema Rais Magufuli.”
JPM: Mpaka sasa tumenunua ndege 6.


1

JPM: Mafanikio ya Tanzania tangu kupata uhuru Desemba 9, 1961, Tumelinda mipaka yetu, wapo waliojaribu kutishia uhuru wetu lakini wameshindwa, hatubaguani kwa misingi ya rangi, kabila, vyama, tumeboreha miundombinu ya reli, barabara, afya na elimu namengine.
Changamoto.
JPM: Licha Umaskini, ukosefu wa huduma za jamii, ajira nakadharika. Tutajitahidi kutatua hizo changamoto ambazo tayari tumeanza kushughulikia.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!