Friday, 16 December 2016

Baba achinja wanaye wawili, ajinyonga

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbrod
Moshi. Mkazi wa Kijiji cha Goha, Kata ya Mamba Miamba, wilayani Same, Kilimanjaro amewachinja watoto wake wawili na kisha kujinyonga kwa kamba.



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbrod Mutafungwa alisema tukio hilo lilitokea Desemba 13, saa tano asubuhi na kumtaja baba huyo kuwa ni Yohana Grason (26) na watoto hao ni Tumaini Yohana (3) na Esther Yohana (6) ambaye alikuwa mwanafunzi wa chekechea.
Akizungumzia tukio hilo, Diwani wa Mamba Miamba, Michael Mauya alisema baba huyo alitekeleza mauaji hayo baada ya kumtaka mkewe aende shambani akisema siku hiyo yeye ndiye atakayewapikia watoto wake uji.
“Lakini baba huyu enzi za uhai wake alikuwa akisema kuwa iko siku ataua tu, maneno yake yametimia sasa na kuamua kufanya kitendo hicho cha kikatili cha kuchinja wanawe,” alisema Mauya.
Hata hivyo, licha ya maelezo hayo, Mauya hakufahamu mara moja sababu za baba huyo kufanya kitendo hicho na hata Kamanda Mutafungwa katika hili alisema, “Chanzo cha mwanamume huyo kufanya mauaji hayo bado hakijajulikana. Tukio hili bado linachunguzwa.”
Kamanda huyo alisema miili ya watoto hao na baba huyo ipo katika Hospitali ya Wilaya ya Same kwa ajili ya uchunguzi wa kidaktari kabla ya taratibu za mazishi kufuata.
Alipoulizwa kuhusu tukio hilo, mtaalamu wa saikolojia kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba Muhimbili (Muhas), Lusajo Kabula alisema kitendo cha mtu kufikia uamuzi wa kuua kinasababishwa na sonono.
“Hii ni hali ya kukata tamaa na kukosa matumaini. Inapofikia hatua hiyo mawazo ya mtu yanampeleka kujiua au kuua wengine au vyote kwa pamoja.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!