Monday 14 November 2016

Trump Akataa Kulipwa Mshahara wa Urais, Afanya uteuzi wa Awali wa Viongozi

donald_trump_gettyimages-150512783_sy9248h
MAREKANI: Rais mteule wa Marekani, bilionea Donald Trump amesema hatakubali kupokea mshahara wa urais pindi atakapokuwa madarakani.
Trump ameweka msimamo huo jana katika mahojiano maalum na mtangazaji maarufu, Lesley Stahl katika kipindi cha 60 Minutes, aliyetaka kufahamu kuhusu uamuzi wake juu ya mshahara wake akiwa ni mfanyabiashara mkubwa.
“Sijawahi kuzungumzia hili, lakini jibu langu ni hapana,” alisema. “Nafikiri inanibidi kupokea kwa mujibu wa sheria $1, kwahiyo ntachukua $1 (Sawa na shilingi 2,200 za Tanzania) kwa mwaka. Lakini hata sijui ni nini,” aliongeza.
Ingawa mtangazaji huyo alimkumbusha Trump kuwa anaiacha $400,000 kwa mwaka, rais huyo mteule alisisitiza, “sitachukua mshahara. Sitapokea.”
Wakati wa kampeni, Trump aliahidi kuwa atajiweka kando na biashara zake endapo atachaguliwa kuwa Rais wa Marekani, na kwamba atajikita zaidi katika kutimiza ahadi zake kwa Wamarekani. Alisema kuwa biashara zake ataziacha mikononi mwa watoto wake.
Reince Priebus
Trump afanya uteuzi wa awali
Mbali na hivyo, Donald Trump, amemteua Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Chama cha Republican, Reince Priebus, kutumika kama Mkuu wa Wafanyakazi.
Bwana Priebus ana uhusiano wa karibu na Spika wa Baraza la Wawakilishi Paul Ryan. Wandishi wa wa habari wanaarifu kwamba uteuzi wa Piebus unaweza kuwaudhi wafuasi wake wa hali ya chini na hii inaashiria kwamba uongozi ujao unalenga kufanya kazi kwa karibu na Baraza la Congress kujihakikishia ushindi wa mapema wa baraza hilo.
Stephen Bannon
Stephen Bannon, alikuwa ni mwenyekiti wa taasisi ya Breitbart News, ambayo ni tovuti yenye maoni ya mrengo wa kulia , naye ameteuliwa kwa nafasi ya mkuu wa mipango na mshauri mwandamizi.
Mkuu wa wafanyakazi ambaye anafanya kazi kama mruhusu na mtengeneza ajenda kwa rais, na kwamba ni mmoja wa chaguo muhimu la mapema kwa rais ajae.
Katika taarifa yake, Trump alinukuliwa akiwazungumiza Priebus na Bannon ni viongozi wenye sifa za hali ya juu waliofanya kazi pamoja wakati wa kampeni zake za kuingia Ikulu ya Marekani.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!