Huduma za usafiri wa ndege zinazidi kushika kasi kwenye mataifa ya Afrika Mashariki kila siku, Kutoka nchini Rwanda nimeipata hii ya Shirika la ndege la Rwanda, RwandAir kununua ndege mpya aina ya Boeing 737-800 Next Gen ambayo inatarajiwa kuongeza ushindani wa safari za anga duniani .
RwandAir imekuwa kampuni ya kwanza barani Afrika na ya pili duniani kununua ndege ya aina hiyo ambayo imewekwa vifaa vya kuwezesha abiria kutumia huduma za intaneti kwa njia ya Wi-Fi.
Ndege hiyo ina uwezo wa kubeba abiria 154 ilitolewa oda ya kununuliwa na Rwanda miaka 6 iliyopita, imetua kwenye uwanja wa ndege wa Kigali November 16, 2016 saa 10 usiku.
Waziri wa uchukuzi wa Rwanda Alexis Nzahabwanimana, amesema ndege hiyo mpya itawezesha shirika hilo kupanua safari zake barani Asia, Ulaya na Marekani.
Mwezi September mwaka huu, Serikali ya Rwanda ilinunua ndege nyingine ambayo ni ya kwanza Afrika Mashariki aina ya Airbus 330-200, iliyopewa jina la ‘Ubumwe’ ikiwa na maana ya Umoja.
John Mirenge, Mkugenzi Mtendaji wa Rwandair’s CEO akiitambulisha ndege hiyo iliyopewa jina la ‘Kalisimbi’.
Dr Alexis Nzahabwanimana, Waziri wa Usafirishaji akizungumza wakati wa mapokezi ya ndege hiyo.
Picha zote kwa hisani a MillardAyo.com
No comments:
Post a Comment