Thursday, 17 November 2016

Rais Magufuli atia saini sheria ya habari


RAIS John Magufuli ametia saini Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016.
Taarifa ya Ikulu jijini Dar es Salaam imesema Rais Magufuli ametia saini sheria hiyo jana ikiwa ni siku 15 baada ya kupitishwa na Bunge la 11 la Tanzania katika Mkutano wake wa 5 Mjini Dodoma.


Aidha Rais amewapongeza wadau wote kwa kufanikisha kutungwa kwa Sheria hiyo.
"Naamini kuwa Sheria hii itasaidia kuboresha sekta ya habari kwa manufaa ya wanataaluma wenyewe na Taifa," alisema Rais Magufuli.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!