Tuesday, 15 November 2016

Polisi wanaoshtakiwa kwa jaribio la kubaka wapata dhamana


Mbeya. Polisi waliofutwa kazi hivi karibuni na kushtakiwa wakidaiwa kujaribu kubaka jana walipata dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya.

Washtakiwa hao, aliyekuwa Konstebo wa Polisi Petro Magana wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) na Konstebo Lucas Ng’weina wa Wilaya ya Kipolisi Mbalizi mkoani Mbeya wanakabiliwa na mashtaka ya kutaka kufanya mapenzi kwa nguvu na wanafunzi wa Sekondari ya Isuto, Wilaya ya Mbeya Vijijini walikokuwa wakisimamia mitihani ya kidato cha nne.
Kwa mara ya kwanza walifikishwa mahakamani hapo wiki iliyopita. Wamepewa dhamana baada ya kutimiza masharti, ikiwamo kuwa na mdhamini mmoja ambaye ni mtumishi wa umma mwenye barua kutoka kwa mwajiri na kusaini dhamana ya maandishi ya Sh7 milioni

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!