Nchini Afrika Kusini mchungaji Lethebo Rabalago wa Kanisa la Mountzion General Assembly lililopo mji wa Limpopo, amekutwa akiwapulizia dawa ya kuua wadudu kwa madai kwamba itawaponya matatizo yao.
Muda mfupi baada ya kusambaa kwa taarifa na picha za Mchungaji huyo akitumia dawa ya kuua wadudu kuwapulizia waumini kanisani kwake, Kampuni inayotengeneza dawa hizo iitwayo Doom imetoa tamko lake na kumuonya mchungaji huyo kuacha mara moja kutumia bidhaa zake kwa matumizi ya aina hiyo.
'Stop spraying our product in people's faces,' Tiger Brands tells #DoomPastor bbc.in/2gelGGh#BBCAfricaLive #SouthAfrica
Na tayari imetoka taarifa kuwa vyombo vya usalama nchini Afrika Kusini vimeanza uchunguzi juu ya tukio hilo la mchungaji.
No comments:
Post a Comment