RAIS John Magufuli jana alitangaza kumpatia bure mfanyabiashara Said Salim Bakhresa zaidi ya hekta 10,000 za ardhi ili alime miwa kwa ajili ya kuzalisha sukari itakayotumika katika viwanda vyake vya vyakula na vinywaji.
Rais Magufuli alisema eneo atakalompa Bakhresa lipo Dar es Salaam na lilikuwa linamilikiwa na wafanyabiashara ambao hawakuwa waaminifu kwa serikali.
“Nipe siku tano tu kuanzia leo, nikazungumze na watu wangu halafu Waziri wa Viwanda atakuletea majibu," alisema Rais Magufuli.
"Nataka ulime miwa ili upate sukari mwenyewe. Kama upo tayari, uniambie na najua umekubali... huwezi kukataa.”
Rais Magufuli alitoa ahadi hiyo baada ya kuridhishwa na jitihada za mfanyabiashara huyo za kuwa na nia ya dhati ya kwenda sambamba na kasi ya serikali ya kuhakikisha Tanzania inakuwa ya viwanda, baada ya kufungua kiwanda cha kusindika matunda cha Kampuni ya Bakhresa.

No comments:
Post a Comment