Sunday, 9 October 2016

CHRIS BROWN AWASILI KENYA ,APASUA SIMU YA SHABIKI,WANANCHI WATAKA AFUKUZWE KAMA KOFFI OLOMIDE


Mwanamuziki maarufu duniani wa nchini Marekani, Chris Brown amewasili jijini Mombasa, Kenya na kujikuta akizua gumzo baada ya kuitupa chini na kuivunja simu ya kiganjani ya shabiki mmoja.




Tukio hilo lililotokea uwanja wa ndege wakati msichana wa Kenya (aliyevaa sketi nyeusi katika picha) alijisogeza kwa Chris Brown ili aweze kupiga naye picha, maarufu kama ‘selfie.’Katika hali ambayo iliwashangaza watu walioshuhudia tukio hilo ikiwa pamoja na waandishi wa habari, mwanamuziki huyo aliichukua simu ya Dada huyo, akaitupa chini na kwenda kupanda gari iliyoandaliwa kwa ajili ya kumchukua.Akihojiwa na vyombo vya habari baada ya tukio hilo, msichana huyo amesema amesikitishwa na kitendo cha Chris Brown ambacho amekiita ni cha udhalilishaji na amesema ataripoti polisi ikiwa ni pamoja na kuharibiwa simu yake.
Habari inayoendelea hivi sasa nchini Kenya ni kuwepo kwa wito kwa wananchi kususia onyesho la mwanamuziki huyo ikiwa ni pamoja na kuzitaka mamlaka za nchi hiyo kumfukuza nchini humo Chris Brown kama zilivyomfanyia Koffi Olomide miezi michache iliyopita. Bofya hapa kutazama video wakati Chris Brown akiwasili katika hoteli aliyoandaliwa nchini Kenya

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!