Jeshi la Polisi limethibitisha kuwa jumla ya askari wake wanne wameuawa usiku wa kuamkia leo baada ya majambazi kuvamia tawi la benki ya CRDB lililopo Mbande, Mbagala wilayani Temeke, Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.
Inadaiwa kuwa askari hao walikuwa wakibadilishana lindo katika Benki ya CRDB, tawi la Mbagala Mmbande na mara wakaibuka watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi na kuanza kuwashambulia kwa risasi na baada ya shambulizi hilo wanadaiwa kuondoka na pikipiki wakielekea maeneo ya Mvuti.
Akizungumza moja kwa moja kupitia kituo cha Redio One Stereo leo asubuhi, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro, amesema watu kadhaa wamekamatawa na msako unaendelea ili kuwapata waliotekeleza unyama huo.
Sirro amesema taarifa kutoka eneo la tukio zinaonesha kuwa majambazi hao walikuwa 14 na baada ya kufanya mauaji hao, walivamia kituo cha polisi cha Mbande kisha wakavunja stoo na kuchukua sare ya askari na silaha.
Akielezea namna tukio hilo lilivyotokea, Kamanda Sirro amesema wahalifu hao walitumia mwanya wakati askari wakibadilishana lindo katika taasisi hiyo ya fedha na kuibuka ghafla na kuanza kurusha risasi.
Kwa mujibu wa Sirro, gari la polisi limechakazwa kwa risasi na askari mmoja aliyekuwa lindo alifanikiwa kukimbia na ndiye aliyeweza kutoa taarifa na maelezo ya namna tukio lilivyofanyika.
Polisi waliouawa ni pamoja na;
E5761 CPL YAHAYA
F4660 CPL HATIBU
G9544 PC TTITO.
No comments:
Post a Comment