Thursday 25 August 2016

Kitwanga aponda ndege mpya za ATCL mwanzo mwisho


Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga jana aliponda aina ya ndege mpya zilizonunuliwa na serikali kutoka Canada kwa ajili ya kufufua Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).


Kitwanga alisema ndege hizo si tu hazina mwendo, lakini pia ilikua ni ajabu kununuliwa kwa fedha taslimu wakati duniani kote ndege hununuliwa kwa kulipa kidogo kidogo wakati mteja akiendelea kuzitumia.

Serikali imelipa kwa Bombardier Aerospace fedha za ndege mbili za Q400 zinazotumia injini ya pangaboi zenye uwezo wa kubeba abiria 70.

Kitwanga ambaye ni mbunge wa Misungwi (CCM), alieleza kushangazwa na kitendo cha serikali kununua ndege hizo ambazo amesema zimetoka katika kampuni ndogo ya mtu binafsi, na kuhoji ubora wake. Aidha Kitwanga alisema Tanzania itakua mteja wa kwanza wa ndege hizo.

Hata hivyo kwa mujibu wa mtandao wa kompyuta wa wikipedia, kampuni hiyo imetengeneza zaidi ya ndege 1,000 za aina hiyo tangu ianzishwe mwaka 1984, na inatarajia kuwa imetengeneza jumla ya ndege 1,192 ifikapo mwisho wa mwaka huu.

Kitwanga alisema hayo wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ilipokutana na ATCL, na Mamlaka ya Usafiri wa wa Anga (TCAA) mjini Dodoma.

Chanzo:
 Nipashe

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!