Saturday 30 July 2016

WATUMISHI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI NCHINI WACHANGIA DAMU SALAMA


zima2Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias  Andengenye (kushoto mstari wa mbele) akiwaongoza Viongozi Waandamizi wa Jeshi hilo kuelekea katika viwanja vya kituo cha Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Ilala eneo lililotengwa kwa ajili ya zoezi la uchangiaji damu salama mara baada ya kuwasili kituoni hapo jana.


zima3Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias  Andengenye akihutubia Maafisa, Askari na watumishi wote wa  Jeshi hilo wakati akifungua zoezi la uchangiaji damu salama ambalo lilishirikisha vituo vyote vya Zimamoto mikoani, ufunguzi huo ulifanyika katika viwanjwa vya Zimamoto na uokoaji mkoa wa Ilala jana.zima1Maafisa, Askari na watumishi wote wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kutoka katika vituo vya Zimamoto Makao Makuu, Chuo, Ilala, Kinondoni, Temeke na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere wakimsikiliza Kamishna Jenerali (hayupo pichani )wakati akihutubia katika ufunguzi wa zoezi la uchangiaji Damu salama lililofanyika katika viwanja vya Zimamoto mkoa wa Ilala.
zima4Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias  Andengenye akichangia damu katika zoezi lililofanyika viwanja vya kituo cha Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Ilala zoezi lililoshirikisha vituo vyote vya Zimamoto mkoa wa Dar es Salaam jana.
zima5Askari na watumishi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakichangia damu katika zoezi hilo jana. (PICHA ZOTE NA FC GODFREY PETER)

KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI THOBIAS ANDENGENYE AMEWAONGOZA VIONGOZI WAANDAMIZI, MAAFISA, ASKARI NA WATUMISHI WOTE WA JESHI HILO KATIKA ZOEZI LA UCHANGIAJI DAMU SALAMA ILI KUTIMIZA DHIMA YA KUOKOA MAISHA YA WATU WANAOPOTEZA MAISHA KWA AJALI ZA MOTO, AJALI ZA BARABARANI, VIFO VYA MAMA WAJAWAZITO WANAOPOTEZA DAMU NYINGI WAKATI WA KUJIFUNGUA NA MAGONJWA MBALIMBALI KAMA VILE UKIMWI, MALARIA, ANAEMIA NA KANSA.
ZOEZI HILI LIMEFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA KITUO CHA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI MKOA WA ILALA  KWA KUSHIRIKIANA NA TAASISI YA MPANGO WA DAMU SALAMA ULIO CHINI YA WIZARA YA AFYA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA WATOTO NA WAZEE.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!