Friday 29 July 2016

Neema yanukia wanajeshi waliopigana Vita vya Kagera





vifaru vya tanzania vikieleka kwenye uwanja wa vita vya Kagera
ASKARI wastaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) walioshiriki vita vya Kagera vilivyomng'oa nduli Idi Amin mwaka 1979 waliopo Mkoa wa Dar es Salaam, wametakiwa kuorodhesha majina yao kupitia wilaya wanamoishi na kuyawasilisha katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.




Agizo hilo lilitolewa jana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, alipokuwa akizungumza na baadhi ya wastaafu wa JWTZ ofisini kwake kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Mjema alisema wastaafu hao wanatakiwa kuwa na ushahidi wa kushiriki vita hivyo ikiwamo nishani ya Vita vya Kagera.
Alisema majina yaandikishwe kupitia ofisi za Muungano wa Wanajeshi Wastaafu Tanzania (Muwawata) za kila wilaya na wenyeviti wa kila wilaya wayawasilishe kwa Mwenyekiti Muwawata Mkoa, Luteni Kanali (mstaafu), Habib Mazome, kabla ya Agosti 2, mwaka huu na Agosti 4, mwaka huu yatawasilishwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Aidha, Mjema alifafanua kuwa wastaafu wawasilishe majina hayo bila kuzingatia kama ni wanachama wa Muwawata.
Hata hivyo, hakufafanua lengo la majina hayo, lakini kwa muda mrefu, wastaafu wa JWTZ waliopigana Vita vya Kagera, wamekuwa wakitoa kilio kwa serikali wakiomba iwaangalie kwa jicho la huruma kutokana na jinsi ambavyo walijitoa mhanga kutetea Taifa lao wakati wa vita hivyo ambavyo vilisababisha baadhi yao kupoteza maisha na wengine ulemavu wa maisha

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!