Saturday 11 June 2016

Watuhumiwa dada’ke Bilionea Msuya waongezeka



Marehemu Aneth Msuya.
Dar es Salaam. Idadi ya watuhumiwa waliokamatwa kuhusiana na mauaji ya dada wa Bilionea Erasto Msuya, Aneth, imeongezeka baada ya kukamatwa watu wawili akiwamo mpenzi wa mfanyakazi wa ndani.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alisema hadi sasa wamekamata watuhumiwa wanne wakihusishwa na mauaji hayo yaliyotokea Mei 26 Mei 26 nyumbani kwake Kibada-Kigamboni, Dar es Salaam.
“Mwanzo tulimkamata mume wa marehemu na msaidizi wa ndani wa marehemu, lakini sasa wameongezeka wengine wawili, akiwamo hawara wa msaidizi wa ndani. Tunaendelea kuwahoji na upelelezi ukikamilika tutawafikisha mahakamani,” alisema Sirro.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!