Sunday 19 June 2016

UGONJWA WA "AJABU" WAUA SITA DODOMA



Dodoma. Watu sita wamefariki dunia katika Wilaya za Chemba na Kondoa mkoani hapa baada ya kuugua ugonjwa usiojulikana.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk James Charles amesema pia ugonjwa huo umeua baadhi ya mifugo katika wilaya hizo.


Alizitaja dalili za ugonjwa huo ni kuhara, kutapika, maumivu ya tumbo, macho kuwa ya njano, kinyesi na matapishi kuwa vyeusi.
Dk Charles amesema walipata taarifa ya kuwapo kwa ugonjwa huo Juni 5, mwaka huu na wagonjwa tisa walitibiwa katika zahanati ya Kijiji cha Mwaikisabe, Wilaya ya Chemba.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!