Tuesday 28 June 2016

Simulizi ya msichana huyu inauma sana!

Msichana simulizi (3)

  Wakonta Kapunda.
Na Imelda Mtema, UWAZI
MSICHANA Wakonta Kapunda (24) anateseka baada ya viungo vyake kupooza kufuatia ajali ya gari iliyompata akiwa Shule ya Sekondari, Korogwe, Tanga.
Akisimulia kisa kizima kwa Uwazi na maisha yake kwa ufupi akiwa nyumbani kwao, Rukwa, Wakonta anasema: “Mimi naitwa Wakonta Kapunda, naishi Mkoa wa Rukwa.



Msichana simulizi (2)


Gari lililomgonga Wakonta Kapunda siku ya mahafari.
“Nilipomaliza elimu ya msingi, nilifanikiwa kujiunga na Sekondari ya Wasichana, Korogwe. Ilikuwa wakati najiandaa kufanya mtihani wa mwisho.
“Nakumbuka ilikuwa mwaka 2012, ndipo nilipopata tatizo hili. Ilikuwa siku ya mahafali (graduation) yangu, mwezi wa pili mwaka huo tukiwa tunajiandaa, mmoja wa wanafunzi aliwasha gari na kuweka reverse kwa kasi hivyo kunigonga mimi pamoja na baadhi ya wanafunzi.
Msichana simulizi (1)
“Hapo ndipo ulikuwa mwanzo wa safari yangu ambayo sijawahi hata kuifikiria kwani nilivunjika uti wa mgongo na kupooza kutoka mabegani mpaka miguuni.
“Katika kutibiwa, ilibidi nipelekwe Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji lakini bila mafanikio.
“Kuanzia hapo, nikawa mtu wa kukaa na kulala tu. Nilijaribu kuyafikiria maisha yangu ya baadaye nikawa naona giza nene mbele.
Msichana simulizi (4)

“Ilifika mahali nikakata tamaa ya maisha lakini Mungu alinisaidia, alinitia nguvu na kunifanya nikubaliane na hali halisi. Najikubali nilivyo na ndiyo maana naweza kufanya mambo ambayo, wengine wanayashangaa sana. mfano, namiliki simu ya kisasa (smart phone) lakini uwezo wa kuitumia sina, inabidi nitumie ulimi kuandikia kwa vile vidole havifanyi kazi inayotakiwa.
“Mwaka huu (2016) lilitokea shindano la kuandika filamu (script). Hili shindano limedhaminiwa na Kampuni ya Filamu ya Maisha ya nchini Uganda.
“Kwa kutumia ulimi wangu huu niliweza kuandika script na kuituma mpaka nikachaguliwa hatua ya kwanza ya mashindano hayo.
“Kikubwa kwa sasa ninachowaomba Watanzania ni kunisaidia kwa njia yoyote niweze kufika Zanzibar tarehe 6, Julai ambako nitatakiwa kukaa kule kwa siku 10. Kutoka kijijini kwetu hadi Zanzibar ni kilomita kama 2620 kwenda na kurudi, gharama ni kama shilingi milioni 4 ambazo sina.
Msichana simulizi (5)
…akiwa na andugu zake
“Nahitaji msaada wa hali na mali kutoka kwa ndugu zangu Watanzania na watu wengine hata kama siyo Watanzania ili niweze kufika kule Zanzibar nikiamini ndiyo safari yangu ya kukuza kipaji changu itakapoanza.”
Kutoa ni moyo wasomaji wa Uwazi. Kwa yeyote atakayeguswa na habari ya mrembo huyu, anaweza kuwasiliana naye kwa kutuma mchango kupitia namba;  0683 886446, jina litasomeka Wakonta Kapunda.
Kama alivyosema, kwa sasa anatumia ulimi kufanya chochote kwenye simu na amejifunza kuperuzi kwa kutumia ulimi baada ya viungo vyake kutofanya kazi isipukuwa kichwa tu.
Anasema japokuwa amepooza mwili wote lakini hajakata tamaa, anaamini ipo siku moja atapona.

Pia amesema kuwa, madaktari walimwambia hawajui ni hospitali gani inaweza kumponesha hivyo kumkatia tamaa kwamba hakuna huwezo wa kuwa sawa tena.


Habari ya mwanafunzi huyo kupata ajali, iliandikwa na Gazeti la Uwazi la Februari, 2012.
Mwanafunzi aliyedaiwa kuwasha gari na kusababisha ajali hiyo, alijulikana kwa jina Kibibi. Mbali na Wakonta, wengine waliopata ajali walikuwa ni Zahra Jumanne (19), Renata Renatus (25), Sophia Godfrey (19), Victoria Mtwale (19), Nancy James (19) na Mwanamkonda Kapunda (19) ambao wote walikuwa kidato cha sita mwaka huo.
Gari hilo aina ya Toyota lenye namba za usajili, T 489 AGJ pia lilimgonga na kumjeruhi mpigapicha maarufu mkoani Tanga, Elias Ngole ‘Ngoswe’. Wote walikimbizwa Hospitali ya Wilaya ya Korogwe, Magunga

1 comment:

Anonymous said...

MUBARAKHA KIMWELI14:51



Allah ampe wepesi wa tiba

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!