Thursday 23 June 2016

POLISI YASHIKILIA WATANO KWA KUNAJISI NA KUUA MTOTO-ARUSHA


POLISI mkoani hapa inawashikilia watu watano kwa tuhuma za kumuua mtoto wa miaka minne baada ya kumnajisi na kumvunja shingo Jumatatu iliyopita.




Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Yusuf Ilembo, alisema wanawashikilia watu hao ambao majina yao hakuyataja na upepelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani.
Ilembo alisema tukio hilo lilitokea Juni 20, saa 3:30 usiku kwenye makaburi ya Baniani yaliyoko Kata ya Unga Limited, jijini hapa.
Alisema baadhi ya watu waliuona mwili wa mtoto huyo ukiwa umetupwa kandokando ya njia ya watembea kwa miguu, karibu na mfereji wa maji umbali wa mita 50 kutoka nyumbani kwao.
Alidai kabla ya kufanyiwa vitendo hivyo, mtoto huyo alikuwa akicheza na wenzake nje kidogo ya nyumbani kwao na ilipofika majira ya saa 12:00 jioni, kwa mujibu wa marafiki zake, alifika mtu mmoja mwanamume.
Walidai kuwa mwanamume huyo alikuwa mrefu na alivaa suruali na kumwambia mtoto huyo amfuate akamnunulie pipi na ndipo alipomfuata na hakurudi tena.
walisema ilipofika majira ya saa 1:30 usiku baada ya wazazi kuona mtoto wao amechelewa kurudi nyumbani, ikiwa si kawaida yake kuchelewa, walianza kumtafuta kwa kuwaarifu majirani pamoja na kutoa taarifa katika Msikiti wa Esso.
Mmoja wa majirani hao alisema baadaye kidogo walipokea taarifa za mtoto kuonekana katika njia ya watembea kwa miguu katika makaburi ya Baniani akiwa amekufa, ndipo walipotoa taarifa kituo cha Polisi Wilaya ya Arusha Mjini.
Alisema polisi waliuchukua mwili wa mtoto huo na kuupeleka Hospitali ya Rufani ya Mkoa ya Mount Meru, kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa daktari na ilibainika alinajisiwa na kuvunjwa shingo, hivyo kusababisha kifo chake.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!