Saturday 18 June 2016

FAHAMU JUU YA MAUMIVU YA MGONGO



Maumivu ya mgongo ni ile hali ya kuhisi maumivu au kutojiskia vizuri/kawaida katika misuli au mifupa ya mgongo wako (eneo lililopo kati ya kiuno na shingo).



Maumivu haya yanatofautiana baina ya mtu na mtu na pia yanategemea sana wapi ilipo shida katika mgongo wako; nini kisababishi na kiungo kilichoathiriwa (kilichoumizwa/jeruhiwa).

Vivyo hivyo dalili nazo hutegemea na kisababishi na hivyo baadhi ya watu huwa na dalili zinazofanana huku wengine wakiwa na dalili za aina mbali mbali kuanzia mamivu ya mgongo, kushindwa kufanya shughuli za kawaida za kila siku kutokana na maumivu, homa na kutetemeka, kupungua uzito (hasa baada ya ajali/magonjwa ya mifupa), kupungua nguvu katika misuli ya miguu, miguu kuwaka moto/kuchomwa chomwa mithili ya sindano au miiba, ganzi kwenye miguu hadi kushindwa kumudu kuzuia haja ndogo na/au kubwa.

Aina kuu za maumivu ya mgongo:
Mara nyingi, maumivu ya mgongo hujitokeza katika aina kuu mbili ambayo ni:
(Maumivu yanayosambaa)
  1. Maumivu yasiyohama (yapo katika eneo la mgongo husika hajalishi unafanya nini - localized pain). Mara nyingi maumivu ya namna hii ni yale yanayokuwa yametokana na kujeruhiwa kwa misuli/mifupa ya mgongo kwa ajali au kupigwa eneo la mgongoni. Au, ni yale yanoyotokanana mkao mbaya usiozingatia afya ya mgongo [anagalia mako mzuri katika somo “post” iliyopita –MKAO MZURI (NI UPI)?] hivyo kusababisha kuchanika kwa misuli ya ndani ya mgongo na kusababisha maumivu!!
  2. Mamivu yanayosambaaa na kuangazia maeneo mengine ya mwili wako mbali na mgongo kama vile miguu. Maumivu haya hutokana na mgandamizo katika mfumo wa fahamu/neva kutoka kwenye mifupa, uvimbe au kuumizwa kwa uti wa mgongo/neva zinazochomozea mgongoni baada ya ajali au kujeruhiwa mgongo wako kwa kupigwa/kuanguka. Mfano: shida ipo mgongoni ila unahisi ganzi kwenye m(i)guu au m(i)guu kuwaka moto).

Visababishi vya maumivu ya mgongo:
(Ubebaji wa mizigo)
  1. Moja ya visababishi vikuu vya maumivu ya mgongo ni aina ya kazi unayofanya. Kazi inayohitaji muda mwingi katika kukaa/kusimama au unaifanya ukiwa katika mkao wa kuinama ni kichocheo cha kupata maumivu ya mgongo.
  2. Mkao: nyumbani, kazini, shuleni, n.k wakati unafanya shughuli zako za kila siku, una nafasi kubwa katika kuongeza au kupunguza hatari ya kupata maumivu ya mgongo [anagalia mako mzuri katika somo “post” iliyopita –MKAO MZURI (NI UPI)?].
  3. Ubebaji wa mizigo mizito (kufikia kilo 5 au zaidi) usiozingatia afya ya mgongo. [Somo la namna ya kubeba mizigo mizito (kufikia kilo tano au zaidi) litakujieni hivi karibuni].
  4. Kulalia godoro laini na lililobonyea/linalobonyea katikati wakati wa kulaa. Hii husababisha misuli ya mgongo kuvutika kupita kiasi wakati umelala na kupelekea kuchanika hivyo kuishia 
    (Godoro la kubonyea)
    katika kupata maumivu ya mgongo na ambayo hudumu kwa muda mrefu (wote) utakokuwa unalalia
      godoro hilo au hata zaidi.
  5. Kujeruhi(wa) mgongo wako kunakotokana na ajali, michezo, kuanguka, kupigwa, n.k au uvimbe (kansa) katika uti wa mgongo.
  6. Ujauzito/uzito wa kupita kiasi (kitambi): wengi wanashtuka wanaposikia kuwa uzito (kitambi) husababisha maumivu ya mgongo, ila akina mama wajawazito wanafahamu! Kinachotokea huwa ni kubadilika kwa mfumo mzima wa maumbile ya mgongo na hivyo kusababisha baadhi ya misuli/mifupa kubeba uzito wakati wa kukaa au kusimam. Kuelemewa kwa misuli/mfupa hii husababisha mabadliko ya mwili katika kutafuta namna ya kufidia hali hiyo… mwisho ni maumivu!!!
  7. Msongo wa mawazo (stress): msongo wa mawazo humfanya mtu kukaa katika mkao mbaya akiwaza na kuwazua hivyo kuishia katika kupata maumivu ya mgongo
    kama nilvyotangulia kusema hapo juu.
  8. Magonjwa yanayoathiri mifupa (pingili) za mgongo kama vile TB ya mifupa ya mgongo na misuli ya pembeni mwa mifupa hiyo na kusababisha maumivu katika eneo husika.
  9. Kuvunjika au kuhama kwa mifupa ya mgogo kutoka nafasi yake ya hapo awali kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo ajali.
    (Msongo wa mawazo)
  10. Umri wa uzeeni: kadri mtu anavyozidi kuukaribia uzee ndivyo kunavyozidi kutokea mabdiliko katika mifumo yote ya mwili ikiwemo ile ya mifupa-na-misuli hivyo kuleta matatizo mengine ya kimfumo yakiwemo maumivu ya mgongo na mengineyo.[Wanawake huwaathiriwa mpema katika uzee wao kuliko wanaume kutokana na mfumo wa vichocheo (homoni) vya miili yao kupungua kwa haraka zaidi baada ya miaka kati ya 45-55 ya umri wao wa kuishi).

Matibabu:
  • Mumivu ya kwaida hasa yale yanayotokana na mshtuko wa misuli ya mgongo au mkao mbaya huwa yanaisha yenyewe ndani ya siku 4 -14, hivo mgonjwa anashauriwa kutumia dawa za kawaida za kutuliza mamivu.
  • Maumivu yanayotokana na kujeruhiwa mgongo ikiwa ni pamoja na ajali/kupigwa/kuangukia mgongo n.k) unashauriwa kufika hospitalini au kituo cha afya kilicho karibu nawe ili upate uchunguzi yakinifu na ushauri/tiba.
  • Maumivu yanayoamabatana na kushindwa kumudu kuzuia haja ndogo na/au kubwa, maumivu makali ya miguu, miguu kuwaka moto/ganzi yanahitaji tiba ya haraka na dharura kwa sababu tayari mfumo wa fahamu/neva utakuwa ulishaguswa/athiriwa kwa namna moja au nyingine.


Namna ya kuzuia maumivu ya mgongo:

(Namna ya kunyenyua mzigo)
  • Mwone daktari wa tiba viungo (PHYSIOTHERAPIST) aliye karibu nawe kwa ushauri kuhusu namna ya:
  • Kukaa vizuri ukiwa nyumbani, kazini au shuleni [anagalia mako mzuri katika somo “post” iliyopita –MKAO MZURI (NI UPI)?].
  • Namna ya kubeba mizigo kwa kujali na kuingatia afya ya mgongo wako ili kuepusha kujeruhi misuli ya mgongo wako.
  • Mpangilio na uboreshaji wa mazingira ya kazi yako ili kuzuia hatari za kupata maumivu ya kimfumo (misuli-na-mifupa)
  • Mazoezi muhimu kwa ajili ya afya ya mgongo wako.
  • Tiba ya mazoezi ya viungo (na mgongo kwa ujumla) inayoendana na shida yako husika.

***Kumbuka, tiba ya mtu mmoja mmoja hutaofautiana kwa kuwa dalili hutofautiana kutokana na kisababishi cha maumivu hayo***

***Usifanye mazoezi uliyoona mwenzako akifanya ukidhani unajitibu kumbe ukawa unaongeza tatizo badala ya kupunguza. Ni vizuri umwone mtaalam akuelekeze tiba stahiki

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!