Friday, 27 May 2016

WENYE SIMU FEKI WASHAURIWA KUZIBADILI KABLA YA KUZIMWA


TCRA imetangaza kuwa Juni 15, mwaka huu, kuwa itakuwa ni siku ya kuzima simu zisizo na viwango.


Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia, alisema kampuni hiyo inayoongoza kwa kuwa na mtandao mkubwa na watumiaji wengi, inaamini kuwa kuna baadhi ya wateja wake wako hatarini kuachwa nje ya mtandao kutokana na kutokuwa na simu zenye viwango vilivyobainishwa na TCRA.
“Natoa wito kwa wateja wetu ambao hadi kufikia sasa hawajaangalia kama simu zao zinakidhi viwango ama wameangalia, lakini hawajachukua hatua ya kununua simu zenye viwango vinavyotakiwa, wafanye hivyo kwa kuwa umebaki muda mfupi kabla ya simu zao kuzimwa na kuwaacha nje ya mtandao,” alisema Mworia.
Katika kuhakikisha wateja wake hawaachwi nje ya mtandao alisema kuwa Vodacom kwa kushirikiana na wadau wanaotengeneza simu, tayari imeingiza simu zenye kiwango cha ubora na gharama nafuu nchini ambazo zinapatikana katika maduka yake yaliyopo sehemu mbalimbali nchini.
“Tusingependa wateja wetu waachwe nje ya mfumo wa mawasiliano na kukosa huduma za mawasiliano, hivyo tutaendelea kufanya kazi na serikali na taasisi nyingine za mawasiliano kuhakikisha Watanzania wanaendelea kupata huduma bora za mawasiliano. Simu zenye viwango na za baei nafuu, zinapatikana kwenye maduka yetu kote nchini,” alisema.
NIPASHE.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!