WATU watatu wamelazwa katika Hospitali ya Missioni ya Mbesa, Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma baada ya kujeruhiwa vibaya na mamba katika matukio tofauti yaliyojitokea hivi karibuni
Hayo yamebainishwa na Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Ires Sekreman, wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu ambapo pamoja na mambo mengine alibainisha kuwa hospitali hiyo imekuwa msaada mkubwa kwa wananchi ambao hukubwa na mikasa ya aina hiyo.
Akifafanua taarifa hiyo, alisema hospitali yake ambayo pia hupokea majeruhi na wagonjwa kutoka katika vijiji vilivyopo nchi jirani ya Msumbiji, imekuwa ikipokea majeruhi wengi kutokana na matukio ya mamba ambao huwajeruhi wakati wakivua samaki na kufanya shughuli mabalimbali katika Mto Ruvuma.
Alimtaja mmoja wa majeruhi hao, Addo Adam (29), mkazi wa Kijiji cha Kazamoyo Tarafa ya Lukumbule wilayani Tunduru mkoani hapa kuwa alilazimika kukatwa mguu wake wa kulia ili kuokoa maisha yake.
Alisema majeruhi huyo ambaye alipokelewa katika hospitali hiyo Aprili 16 mwaka huu, mguu wake uliharibika vibaya kutokana na kutafunwa na mamba na kwamba kama usingekatwa ungeoza jambo ambalo lingemsababishia kupoteza maisha. Majeruhi mwingine alimtaja kuwa ni Sharif Alli Makunga.
Akizungumzia matukio hayo Kaimu Afisa Wanyamapori wa Wilaya ya Tunduru, Peter Mtani, pamoja na kudhibitisha kuwapo kwa matukio hayo, alisema Machi 18, mwaka huu, Zainabu Nakale Kopwe, alipoteza maisha kutokana na kushambuliwa na mamba wakati akiwa anaoga.
Akifafanua taarifa hiyo Mtani alisema kuwa chanzo cha matukio hayo kinatokana na jamii kuutegemea mto huo kuendesha shughuli zao za kila siku.
Alisema katika matukio yote yaliyoripotiwa na ambayo idara yake haikuyapata, huwatokea wakati wakiwa wanaoga, kuchota maji kwa ajili ya kunywa, kwenda kufua na wengine wakivua samaki.
NIPASHE

No comments:
Post a Comment