Na Ripota maalum, Dar
UKIHADITHIWA
na kuonyeshwa chumba cha Dereva Tax anayeonekana kitaani na katika kazi
zake akiwa amepiga pamba wala hutaamini masikio yako wala macho yako
pindi utakapopata bahati ya kufika na kushuhudia chumba hicho kilichopo
maeneo ya Gold Star Mtaa wa Mbezi Mtoni Bondeni jijini Dar es Salaam.
Mtandao
huu ulipata fursa ya kufika na kushuhudia yale yaliyokuwa yakisemwa na
baadhi ya wakazi wa mtaa huo jana majira ya saa tano usiku baada ya
kutokea mtafaruku na sintofahamu katika nyumba hiyo ya Mama Mwakajinga,
anayoishi Dereva huyo aliyejulikana kwa jina la Steven al-maarufu kama
'NYATI'.
Hivi ndivyo hali ilivyo ndani ya chumba hicho.
Akizungumza
na mtandao huu, Mama mwenye nyumba kuhusu tukio hilo, alisema kuwa siku
ya Mei 23, akiwa ameketi uwanjani karibu kabisa na Chumba cha Jamaa
huyo huku akichambua mboga, alihisi harufu kali na mbaya iliyokuwa
ikivuma kutoka chumbani kwa Dereva huyo aliyepanga katika nyumba yake
tangu mwaka 2008 na kuona wadudu aina ya funza wakitoka chumba hicho
kupitia chini ya mlango.
Kesho
yake Mei 24 Baada ya kuona wadudu hao huku harufu ikizidi kuwa kali,
alimuita jirani yake na kumshirikisha jambo hilo huku wote wakishikwa na
butwaa na kuwa na mashaka na chumba hicho.
Vyupa kila kona
Mei
25 Mama mwenye nyumba aliamua kwenda kwa Mjumbe wa eneo hilo Badili
Makoye, kutoa taarifa juu ya wasiwasi uliotanda katika nyumba hiyo na
kuongozana na Viongozi wengine, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo,
Frank Kyaruzi, Wajumbe wengine Abdalla Mlaliya na Matrida Paston,
waliofika na kujionea hali halisi ya chumba hicho.
Baada ya viongozi hao kufika eneo la tukio walimuamuru Mama mwenye nyumba kwenda kutoa taarifa kituo cha Polisi.
Mama Mwenyenyumba hiyo, akiongoza zoezi la kufungua chumba hicho.
Mama
huyo alitekeleza agizo na kwenda kuripoti Kituo cha Mbezi Garden na
kuongozana na Mkuu wa Kituo hicho na baadhi ya askari hadi nyumbani na
kukuta hali hiyo ya sintofahamu.
Walipofika
eneo la tukio na kushuhudia hali hiyo, Mkuu wa Kituo aliamuru mlango
huo uvunjwe huku wanachi na Viongozi wa Mtaa huo wakishuhudia na kuingia
ndani ambako walikuta Chumba kizima kikiwa kimejaa Chupa za Plastiki
zilizojaa mikojo, Mifuko ya Rambo ikiwa na Vinyesi, Feni moja
iliyochomekwa kwenye Soketi ya Umeme ukutani, Pakiti nyingi tupu za
Sigara aina ya Embassy na Kondomu zilizotumika na zisizotumika.
Baada
ya zoezi hilo, Mwenyenyumba alimpigia simu mpangaji wake na kumtaka
kurejea nyumbani, lakini Dereva huyo alijibu kuwa kwa muda huo alikuwa
mbali maeneo ya Kunduchi na kuahidi kuwagongea usiku pindi atakaporejea.
Hadi
Mtandao huu unaondoka eneo la tukio majira ya saa tano usiku bado
wakazi wa maeneo hayo walikuwa wamejazana nje ya Chumba hicho
wakiendelea kumsubiri arudi ili kupata ukweli kuhusu mambo waliyoyaona
katika chumba chake.
Aidha
Mama mwenye nyumba aliuambia mtandao huu kuwa mpangaji wake huyo, tangu
alipohamia katika nyumba hiyo mwaka 2008, hakuwahi kumuona akiingia na
mwanamke katika chumba hicho, wala kumuona mgeni wa aina yeyote kwa
Dereva huyo,jambo lililomshangaza kukuta Kondom zilizotumika katika
chumba hicho. Ama kweli ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Filauun
No comments:
Post a Comment