Saturday 16 April 2016
SAID LUGUMI- SI KILA JIPU NI LA KUTUMBULIWA!
Hatimaye mmiliki wa kampuni yaLLugumi Enterprises Ltd ndugu Said Lugumi ameibuka kutoka mafichoni na kuonya kuwa siyo kila jipu linatumbuliwa.
Aidha bwana Lugumi amewahasa watanzania waache kufanya mambo kwa hasira kwani kila jambo limepangwa vyema kwa wakati wake. Hayo aliyasema jana wakati akifanya mahojiano na gazeti la Tanzania Daima.
Katika hatua nyingine waziri wa mambo ya ndani ndugu Charles Kitwanga ameonya kuwa mambo yote yanayohusu mkataba wa Lugumi yalitoka ngazi ya juu bila kufafanua ni ngazi ipi.
Ndugu Said Lugumi kupitia kampuni yake ya Lugumi Enterprises Ltd mwaka 2011 alipewa zabuni ya kusambaza vifaa maalum vya kuchukua alama za vidole kwenye vituo vyote vya jeshi la polisi nchini inayogharimu Tshs bilioni 37 ambapo tayari amelipwa Tshs bilioni 34 huku utendaji kazi wake ukiwa chini ya asilimia kumi.
"Watanzania mnapenda sana udaku na uongo uongo. Mtu kasajili kampuni kihalali, kaomba tenda kihalali, kaipata kihalali, kalipa kodi halali kaingia mkataba halali kautendea haki mkataba wake mpaka upande wa pili ukaridhika na kaondoka kihalali kwa pasipoti na documents zote, mbele ya uwanja wa ndege ulio chini ya jeshi, polisi, uhamiaji na maafisa wa usalama kibao. Sasa hii hadithi katoroka inaanzia wapi? Tafakari. Sio kila jipu ni la kutumbua na hata mtumbuaji anajua. Huu mchezo hauhitaji hasira wala jazba."Aliema Lugumi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment