Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) inakabiliwa na uchache wa madaktari bingwa wa upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu ambapo mpaka sasa kuna madaktari nane nchi nzima.
Akizungumza wakati wa kuzindua kozi ya wiki moja ya upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu iliyofanyika leo asubuhi katika ukumbi wa Millenium Towers, Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema nchi ina wataalamu wachache katika fani hiyo ambapo mmoja yupo Hospitali ya Bugando huku saba wakihudumia MOI.
“Kubwa tunalojifunza hawa ambao ni wachache wataweza kujengewa uwezo ili kuweza kujua changamoto na mahitahi ya sasa katika kufanya upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu na serikali tumeahidi tutaongeza wataalamu katika fani hiyo na kununua vifaa vya kisasa vya CT Scan na MRI ili kuwaongezea ufanisi,” alisema Ummy
No comments:
Post a Comment