Imeelezwa kuwa Jiji la Dar es salaam linaongoza kwa upangaji holela wa makazi hivyo basi litapangwa upya kutokana na Mpango mji utakayokamilika mwezi Julai.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kikao cha kazi kati ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi na Wadau wa sekta ya Uendelezaji Milki amesema kuwa Jiji la Dar es salaam limekaa vibaya halina mpangilio hivyo kupitia wizara yake mwezi Julai Mpango mji utakuwa tayari na Jiji litakaa sawa.
“Kwa sasa tumeanza kuweka sawa majiji ya Arusha na Mwanza ila Dar es salaam inaongoza kwa mpangilio mbovu kwani watu wamejenga kiholela hivyo kuanzia mwezi wa saba Master Plan (mpango mji) utakuwa umekamilika hivyo kila kitu kitu kitakuwa sawa”. Alisema Lukuvi
Aidha Waziri Lukuvi amewataka wadau wa sekta binafsi wajenge nyumba ambazo Mtanzania wa kipato cha chini aweze kumiliki kwani kwa sasa nyumba zinazojengwa sio kwa ajili yao bali zinalenga wenye uwezo mkubwa.
Sanjari na hayo Lukuvi amesema kuwa Kupitia Sheria itakayoundwa kusimamia mpango mji pia kitakuwepo kipangele cha kutetea haki za wapangaji kwani kwa sasa kila mmoja anapangisha nyumba kwa bei anayojisikia yeye kwakuwa hakuna chombo kinacho wasimamia wapangaji.
No comments:
Post a Comment