Saturday 16 April 2016

DARAJA LA KIGAMBONI LIMEANZA KUTUMIKA LEO

April 16 2016 ni siku ya kwanza kwa wakazi wa kigamboni kuanza kutumia Daraja jipya lakigamboni, kuvuka kutoka upande wa vijibweni kwenda upande wa pili wa kurasini Daraja la kigamboni litafunguliwa rasmi siku ya tareheApril 19 2016 na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John pombe Magufuli

IMG-20160416-WA0026
IMG-20160416-WA0027
IMG-20160416-WA0028
IMG-20160416-WA0029
IMG-20160416-WA0030
IMG-20160416-WA0031
IMG-20160416-WA0032
IMG-20160416-WA0033
IMG-20160416-WA0034
IMG-20160416-WA0035
IMG-20160416-WA0036
IMG-20160416-WA0038
IMG-20160416-WA0039
IMG-20160416-WA0041
IMG-20160416-WA0042
IMG-20160416-WA0044
IMG-20160416-WA0045
IMG-20160416-WA0046
IMG-20160416-WA0047
IMG-20160416-WA0051
IMG-20160416-WA0050
IMG-20160416-WA0048
Kama siku ya leo imekupita ujaenda kupita kwenye daraja jipya la kigamboni kuna haya mambo matano ya kufahamu kuhusu Daraja la Kigamboni Dsm baada ya kuanza kutumika leo.
1. Kwenye eneo la daraja hili kuna kituo cha Polisi chenye mpaka mahabusu hivyo yeyote atakaezingua itakua rahisi kumshughulikia, pia kutakuwa na mizani ya kupimia magari mazito pamoja na ofisi ya kulitazama au kufatilia Daraja litakapoanza kutumika.
2.Watakaokuwa wanapita kwa kutumia vyombo vya moto watakuwa wanalipia kuvuka kupitia daraja hilo ndio maana kuna ofisi au ‘vijiwe’ maalum ambavyo vitakua vinafanikisha process zote za kulipia.
3. Baada daraja kuanza kutumika rasmi, Injinia anaesimamia ujenzi huo ameomba Watanzania kujali na kuthamini kila kilichopo kwenye daraja hilo na sio kuiba au kuharibu chochote, tayari mpaka sasa Camera nne za video za kurekodi mienendo na usalama wa daraja hilo zimeibiwa.
4.Ujenzi wa daraja hili ulianza February mwaka 2012 na walitarajia wangemaliza ujenzi January 31 2015 lakini ikashindikana sababu Wajenzi walipata changamoto katikati ya bahari, walichimba chini ya kitako cha bahari mita kama sitini na nne lakini walipofika kwenye mita 56 wakagundua kulikua na pango chini, wakaendelea kwenda chini mita 84.
5.Gharama za ujenzi kwa Mkandarasi ni shilingi za kitanzania BILIONI 214.6 ambazo kimkataba asilimia 25 zinalipwa kwa pesa za Kitanzania na asilimia 75 zinalipwa kwa dola za Kimarekani ambapo wakati wanafungua tenda Dola ya kimarekani ilikua shilingi 1590.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!