Tuesday, 19 April 2016

ATOLEWA NDANI YA NDEGE KWA KUONGEA KIARABU



Mwanafunzi wa chuo kikuu raia wa Iraq katika jimbo la California nchini Marekani anasema kuwa alitolewa kutoka ndege ya shirika la ndege la Southwest baada ya kufanya mazungumzo kwa lugha ya kiarabu.

Shirika hilo la Southwest lilisema kuwa Khairuldeen Makhzoomi aliondolewa tarehe 9 mwezi Aprili baada ya ndege hiyo kupaa.
Bwana Makhzoomi anasema alikuwa akizungumza na mjomba wake kwa njia ya simu kuhusu hotuba ya katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon.
Bwana Nmakhzoomi anasema kuwa mwanamke mmoja kwenye ndege hiyo alimkodolea macho wakati alitumia jina "inshallah" akimaanisha Mungu akipenda.
Baada ya kutumia jina hili mfanyikaziawa shirika la Southwest alimsindikiza nje ya ndege.
Bwana Makhzoomi ambaye aliingia nchini Marekani kama mkimbizi kutoka Iraq na sasa ni mwanafunzi wa chuo cha Carlifonia cha Berkeley , aliambiwa kuwa hawezi kuingia kwenye ndege hiyo.

BBC.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!