Moja ya sekeseke langoni mwa United, lakini walifanikiwa kuondosha hatari na kufanikiwa kutoka na ushindi wa moja bila
Bao la mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na kiungo wa Manchester United Juan Mata uliiwezesha Man Utd kuibuka na usindi wa bao moja bila ya majibu katika uwanja wao wa nyumbani ( Old Traford ).
Juan Mata akifunga bao kwa mkwaju wa adhabu ndogo
Bao hilo lilipatikana katika dakika za majeruhi dakika ya 83, baada ya kufanyiwa madhambi kwa Antony Martial umbali wa yadi 20 kutoka langoni mwa Watford Mata aliikunja vizuri mpira huo wa adhabu ambao ulimshinda mlinda mlango wa Watford Haurelho Gomes.
Kocha wa Man Utd mdachi Luis Van Gaal maarufu kama King Lui akifananishwa na mfalme wa ufaransa kutokana na majina yao alianzisha kikosi cha vijana wengi katika kikosi chake kama ilivyokuwa dhidi ya Arsenal na cha mafanikio zaidi ni kwamba Van Gaal alimuanzisha beki wa kati Mghana Timothy Fosu-Mensah ambaye alionekana kummudu vilivyo mshambuliaji hatari na mfungaji bora wa Watford Odion Ighalo ambaye alionekana kuisumbua vilivyo ngome ya mashetani hao wekundu ila safu ya ulinzi ya United ilibaki kuwa imara ikiongozwa na kipa Degea ambaye ndiyo amekuwa chachu ya mafanikio ya United.
Marcus Rashford akimtoka mchezaji wa Watford katika mpambano ulifanyika Old Traford.
Mashabiki wengi wa Man Utd wakikuwa wakijiuliza juu ya mshambuliaji wao hatari ambaye ndiyo kwanza kwa walio wengi wanaanza kumfahamu akiwa ametokea kikosi B cha mashetani hao naye si mwingine bali ni kinda wa miaka 18 Marcus Rashford ambaye amejipatia umaarufu hasa nchini Tanzania kwa taswira ya kufanana na jamii ya watu wa kisiwa cha Zanzibar na kumpachika jina la mpemba, kijana amefanya mambo makubwa kiasi kwamba nadhani anaanza kuwatishia amani baadhi ya washambuliaji wa klabu hiyo, akiwemo mkongwe Wayne Rooney,
Kijana Rashford ameonekana kubadilisha kabisa mipango ya kocha Van Gaal ya kutaka kumbadili Rashford ili aingie Jesse Lingard ambayo ndiyo mabadiliko ambayo yanaweza kuingia akilini ili Antony Martial aingie pale kati kama mshambuliaji wa mwisho ila mambo yalibadilika pale kilipoanza kipindi cha pili baada ya kumpeleka pembeni Rashford alionekana kumudu hata akiwa mshambuliaji wa pembeni na kuleta tafrani kubwa sana langoni mwa Watford kiasi cha kumfanya kocha Van Gaal kumbadili kiungo wa kati Ander Herera na nafasi yake kuchukuliwa na Lingard.
Mpaka sasa Man Utd inashika nafasi ya tano nyuma ya Man city zikiwa zote zina pointi 47 isipokuwa United ina michezo mingi na City pia ina wastani mzuri wa magoli.
Wakati Man Utd wakisherehekea ushindi wao huo kwa mahasimu wao wa London hali ilikuwa tofauti baada ya kukubali kipigo cha mabao mawili kwa moja kipigo ambacho kinamuweka kocha mkuu wa timu hiyo mzee Arsene Wenger kuwa katika wakati mgumu katika mbio za ubingwa huo Arsenal ambayo imepata vipigo vitatu mfululizo hadi sasa baada ya kupigwa na Barcelona pia dhidi ya Manchester United na leo dhidi ya Swansea City.
Arsenal ilianza vizuri baada ya kufanikiwa kupata goli la kuongoza kupitia mshambuliaji wake chipukizi Joel Campel katika dakika ya 15 ya kipindi cha kwanza bao lilidumu mpaka dakika ya 32 pale Wayne Routledge alipoisawazishia Swansea, hadi mapumziko mabao yalikuwa moja kwa moja
Joel Campell akifunga dhidi ya Swansea
kipindi cha pilia kilianza kwa kasi huku kila timu ikimshambulia mwenzie huku Arsenal ikishambulia zaidi kwa ajili ya kutafuta bao la pili na la ushindi, wakikoki kila aina ya bunduki waliyokuwa nayo ilimradi waweze kupata bao la pili, lakini risasi zao zilionekana kugeuka kuwa maji mbele ya bata maji kutoka Wales, mnamo katika dakika ya 74 alikuwa Ashley Williams aliyeipatia Swansea goli la pili na la ushindi na kuifanya Swansea kuondoka London zikiwa na pointi tatu muhimu
Routledge akifunga goli lakusawazisha dhidi ya Arsenal
Ashley Williams akishangilia goli lake na ushindi dhidi ya Arsenal
Wakati hayo yanatokea kwa hayo yanatokea kwa Arsenal majirani zao Liverpool maarufu kwa jina majogoo wa jiji la London wamefanikiwa kuwika kabla ya Alfajiri na kufanikiwa kuifunga Man City kwa jumla ya mabao matatu kwa sifuri mabao ambayo yalikfungwa na Adam Lalana na la pili kuwekwa kimiani na mchezaji aliyeuzwa kutoka Man City kwenda Liverpool kiungo James Milner na la Tatu kufungwa na Roberto Firmino
Katika matokeo mengine katika EPL Tottenham Hotspurs wamekubali kipigo cha goli moja bila ya majibu goli lililofungwa na Antonio na kuifanya Westham United kuzibakisha point zote tatu muhimu kwa wagonga nyundo hao wa London, Pia goli la Shakiri limeizamisha Newcastle kwa kukubali kipigo cha bao moja bila majibu dhidi ya Stoke City na kuwafanya waendelee kuwa chini ya msimamo huo wa ligi ya England.
No comments:
Post a Comment