
Leo ni siku ya wanawake duniani, bila kusahau wanawake wenzetu ambao wako vijijini na changamoto wanazozipata katika kuendesha maisha yao ya kila siku.
wanawake vijijini changamoto hizi zimekuwa ni maradufu ukilinganisha na zile za wanawake wanaoishi mjini na wenye fursa mbalimbali.

Kupitia matukio na ishara mbalimbali nchi nyingi zimekuwa na maadhimisho maalumu kwa ajili ya kumkumbuka kila mwanamke duniani na kutafakari kwa kina mchango na umuhimu wake katika uwepo wa dunia na mwendelezo wa maisha.
Tanzania ni miongoni mwa Mataifa ambayo yamekuwa mstari wa mbele kutambua mchango wa mwanamke na kuthamini jitihada zake katika kuleta mafanikio na kuhamasisha mabadiliko ya jamii nzima na kwake pia.
Inatambua pia, umuhimu wa mchango wa mwanamke katika shughuli za kisiasa, kijamii na kiuchumi. Kwa sababu hiyo mwaka huu inaungana na nchi nyingine duniani kuadhimisha siku ya wanawake duniani, kwa pamoja zikibeba ujumbe mkuu “Shirikisha Mtoto wa kike, chochea Maendeleo”
Wanawake ndio wazalishaji wakubwa.
mama anaweza kuweka ushawishi usiolinganishwa na mtu mwingine yeyote katika uhusiano wowote. Kwa nguvu ya mfano wake na mafunzo, wanawe hujifunza kuheshimu uanawake na kujumuisha nidhamu na maadili ya hali ya juu katika maisha yao. Mabinti zake wanajifunza kufurahia na kukuza uadilifu wao wenyewe na kusimama kwa ajili ya kilicho sahihi tena na tena, ijapokuwa haina sifa. Upendo na mategemeo makubwa ya mama huwaongoza watoto wake kuishi na kutenda bila visababu kuwa makini kuhusu elimu na maendeleo binafsi, na kutoa michango endelevu kwa wema wa wote walio karibu nao.
Kama bibi, mama na vioo vya jamii, wanawake wamekuwa ni walezi wa kiini cha maisha.
















No comments:
Post a Comment