Tuesday, 8 March 2016
KUTOKA KWA SUPER WOMAN JOYCE KIRIA
Usipende kutafuta sababu za kuhalalisha uvivu wako. wanasema siku zote maisha ni kuchagua. ukichagua kufanikiwa utatafuta njia, ukichagua kushindwa utatafuta sababu... Fanya kazi ungali bado kijana una miguvu kibao, fanya kazi kwa nguvu zako zote, kwa akili yako yote na maarifa yote. Usipoteze muda, maisha hayakusubiri.
muda haukusubiri, uzee unakujia. utafika wakati mwili utakuwa umechoka na hutaweza kukimbia kama sasa... Acha kulalamika na kunung'unika una fursa kubwa sana ya kubadili maisha yako kuwa bora zaidi ya hapo ulipo. Wajibika jitume hakika hutajuta... Uwe na wiki ya mafanikio tele
Subscribe to:
Post Comments (Atom)














No comments:
Post a Comment