Friday 12 February 2016

TATIZO MUHIMBILI NI MAJENGO SIO VITANDA



Siku moja baada ya Rais John Magufuli, kuvamiwa na kundi la wanawake Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakimtaka atatue kero ya wazazi kulala chini, imebainika tatizo si vitanda wala  magodoro, bali ni eneo la kuviweka.

Mkurugenzi wa Wauguzi na Ubora Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Agness Mtawa, aliyesema hayo  jana wakati akizungumza na Nipashe, huku akiongeza kuwa, jumla ya vitanda vipya 50 na magodoro 40 vipo stoo baada ya kukosa eneo la kuvipanga.
“Wingi wa wagonjwa na uwezo wa hospitali ni vitu viwili tofauti, mfano wodi 37 vitanda vilivyopo ni 33 lakini wagonjwa kwa leo ni 63 na wodi namba 33 vitanda vilivyopo ni 33 huku wagonjwa wakiwa ni  56, kwa nini watu wasilale kwenye magodoro,” alisema na kuongeza:
“Tena wagonjwa wanaongezeka kutokana na msimu, Machi na Aprili hulala kwenye magodoro hadi kufikia mlangoni, hatuwezi kumkataa mgonjwa anapoletwa hapa, tunawapokea wote na kuwahudumia, haiwezekani mjamzito anafika mapokezi yupo kwenye hatua ya mwisho ya kujifungua eti tumrudishe kisa kitanda, tutamhudumia tu,” alisema.
Alisisitiza kuwa, ili kumaliza tatizo hilo lazima kuongezwe majengo mengine kwa sababu yaliyopo hayaendani na idadi ya wagonjwa wanaopokelewa kila siku.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!