Thursday 18 February 2016

MOJA KWA MOJA: Uchaguzi mkuu Uganda

Mbabazi

15:47 Upigaji kura katika kituo cha Ggaba, Kampala umesitishwa baada ya makabiliano kati ya polisi na wapiga kura.
15:16 Rais Yoweri Museveni, anayewania urais kupitia chama cha NRM, amepiga kura yake katika kituo cha shule ya upili ya Kaaro, gazeti la Daily Monitor linaripoti.


14:34 Mgombea urais Amama Mbabazi ameandika kwenye Twitter: "Nimetekeleza wajibu wangu kama raia mwema na kupiga kura yangu katika uchaguzi huu wa urais wa mwaka 2016."
Baadaye akaongezea: "Mimi na mke wangu Jacqueline tumemaliza kupiga kura. Nimefahamishwa kwamba baadhi ya vituo vilianza upigaji kura adhuhuri. Tafadhali, kuweni na subira na mpige kura."
MbabaziImage copyrightAmama Mbabazi Twitter
Image captionAmama Mbabazi amepiga kura yake eneo la Kanungu
14:00 Msemaji wa Tume ya Mawasiliano ya Uganda Jotham Taremwa asema hana habari kwamba tume hiyo ilitoa agizo la kufungwa kwa mitandao ya kijamii ya Twitter, Facebook na Facebook kama inavyoripotiwa katika vituo vingi vya habari. Amesema hayo kwenye mahojiano na kituo cha runinga cha NTV.
13:00 Tume yahimiza utulivu
Kupitia taarifa, Tume ya Uchaguzi imekiri kwamba matatizo ya kucheleweshwa kwa upigaji kura yamekumba maeneo ya Wakiso na Kampala. Hata hivyo, imesema matatizo hayo yametatuliwa na uchaguzi ukaanza maeneo mengi. Imewahimiza wananchi kuwa watulivu.
Imeahidi wapiga kura watakaokuwa vituoni kufikia saa kumi alasiri wataruhusiwa kupiga kura.
12:48 Mwandishi wa BBC Charlotte Attwood amekuwa katika kituo kimoja cha kupigia kura eneo la Nansana, karibu na Kampala ambapo ameona lori likisafirisha masanduku ya kutumiwa kupigia kura, licha ya kwamba upigaji kura ulifaa kuanza saa tano awali.
12:32 Usishangae beseni ni za nini vituoni. Zinatumiwa na wapiga kura kujaza chaguo lao kwenye karatasi ya kura.
12:19 Katika vituo vingi, kuna milolongo mirefu ya watu. Wachuuzi wametumia hii kama fursa ya kujipatia posho. Kama mwanamke huyu anayewauzia wapiga kura maji eneo la Mbale, mashariki mwa Uganda. Anauza kila pakiti ya maji Sh100 za Uganda ambazo ni sawa na senti 3 za Marekani.
11:50 Mpinzani mkuu wa Rais Yoweri Museveni, Dkt Kizza Besigye, amepiga kura yake, gazeti la serikali la New Vision linaripoti.
11:28 Mwanamume huyu alikuwa miongoni mwa wapiga kura wa kwanza kumaliza kupiga kura katika kituo cha Mbale. Anaonyesha kidole chake kilichopakwa wino.
11:20 Mwanamke akitumbukiza kura yake kwenye kijisanduku mjini Mbale, mashariki mwa Uganda.
10:40 Katika baadhi ya vituo, upigaji kura bado haujaanza kutokana na kuchelewa kwa karatasi na vifaa vya kupigia kura.
09:56 Magazeti ya Uganda yameongoza na habari za uchaguzi.
07:45 Upigaji kura katika maeneo mengi umeanza, ingawa kwa kuchelewa. Hapa ni Kalangala watu wakipiga kura.
07:44 Kuna ripoti kwamba baadhi ya watu wanaotumia simu kuingia mitandao ya kijamii ya Twitter na Facebook wanatatizika. Lakini WhatsApp inafanya kazi.
07:30 Upigaji kura ulifaa kuanza saa moja asubuhi lakini katika vituo vingi, licha ya wapiga kura kujitokeza, shughuli yenyewe haijaanza na wapiga kura wanalalamika. Katika kituo cha Kamwokya Central Market, vifaa vya kupigia kura vinaingizwa kituoni pole pole. Mwangalizi wa uchaguzi wa Jumuiya ya Madola Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo amekuwa katika kituo hicho.
Obasanjo
Image captionBw Obasanjo anaongoza waangalizi wa Jumuiya ya Madola
07:09 Tuangalie takwimu muhimu kuhusu uchaguzi wa Uganda unaofanyika leo.
Takwimu muhimu
Wagombea urais8
Maeneo bunge290
Vituo vya kupigia kura28,010
Wapiga kura waliosajiliwa15,277,196
07:00 Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa.
CHANZO: BBC

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!