Saturday 2 January 2016

WAZIRI MKUU AKAMATA MAJIPU YA KUTUMBUA KIGOMA


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa aliyesimama akizungumza katika kikao chake cha majumuisho ya ziara yake mkoani kigoma kilichofanyika ukumbi wa NSSF, Kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Issa Machibya, katikati ni Mwenyekiti wa CCM Amani Warid Kaboulou na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Eng. John Ndungulu.


Ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, mkoani Kigoma imewaacha matatani baadhi ya viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji, baada ya kubaini uuzwaji wa majengo ya Halmashauri kinyume na taratibu.

Majengo hayo ni pamoja na jengo la Kigodeco, Jengo la Mwanga Center, viwanja 16 pamoja na msitu wa masanga, hali iliyosababisa Waziri Mkuu kutoa agizo kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Mhandisi John Ndungulu kusimamie  mchakato wa ufuatiliaji wa tuhuma hizo mpaka itakapofika Januari 2, 2016  ambapo atatakiwa kuwasilisha ripoti katika ofisi ya Waziri Mkuu.


 Waziri Mkuu Majaliwa alitoa kauli hiyo hii leo kwenye kikao cha majumuisho ya ziara yake ya  siku tatu mkoani  humo katika ukumbi wa NSSF, ambapo alisema kuwa uchunguzi unaonyesha uuzwaji wa mali hizo za umma haukuwa wa kiharari.



Awali uzwaji wa majengo ulisitishwa na uongozi wa Mkoa kwa kuwa mali hizo ni sehemu ya mali ya umma, lakini licha ya kusitishwa huko Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji, Boniface Nyambele kwa kushirikiana na madiwani wa Halmashauri hiyo waliuza  mali hizo.

“Leo Mkurugenzi na Mhandisi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji mtaenda kwa Katibu Tawala wa Mkoa na kutoa maelezo kwa maandishi kuhusu mchakato mzima wa uuzwaji wa majengo na viwanja hivyo kwa bei ya kutupa” aliagiza Waziri Mkuu Majaliwa.
Baadhi ya viongozi wa Wilaya za Mkoa wa Kigoma wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (hayupo pichani) katika kikao cha majumuisho ya ziara yake mkoani hapa.
 Aidha baadhi ya Madiwani walikuwa katika mchakato huo Asha Omari na Mgeni Kakolwa kwa nyakati tofauti walikiri majengo kuuzwa kwa utashi wa  Mkurugenzi  wa Halmashauri akishirikiana na aliyekuwa Meya wa Manispaa hiyo  Bakari Beji na Naibu wake  Rashidi Ruhomvya.



“Mwezi wa saba tuliitwa katika kikao cha dharura lakini ajenda za kikao hatukuzifahamu, baada ya kuingia tukakuta ajenda ya kuuzwa kwa mali hizo, tulivutana baina ya madiwani wa CCM  na CHADEMA, lakini kwakuwa madiwani wa CCM tulikuwa wachache ajenda hiyo ilipitishwa  na kuuzwa kwa mali hizo za umma” walibainisha Madiwani hao.

Kwa mujibu wa madiwao hao, jengo la Kigodeco liliuzwa kwa kiasi cha shilingi milioni 375 ambapo katika fedha hizo,kiasi cha  cha milioni 167 zirirudishwa kwa mzabuni aliyekuwa amekodisha jengo hilo baada ya kukatisha mkataba na sh.milioni 100 walidai wanawekeza katika ujenzi wa maabara wa shule za skondari za manispaa hiyo. 

Wakati huohuo kiongozi mmoja wa manispaa hiyoambaye hakupenda jina lake litajwe alisema kuwa,  skendo hiyo ina mikono mingi ,kwa kuwa mkurugenzi hawezi kuuza bila kushirikiana na wenzake ambao walianzisha mchakato huo na shida kubwa ni kutokana na utashi wa siasa.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!