Wakati vijana wengi tumekuwa tukilalamikia juu ya tatizo la kutokuwepo kwa ajira hali inayosababisha umaskini mkubwa miongoni mwa vijana wengi, huku kumekuwa na ongezeko la vijana wengi wanaohama vijijini na kuhamia mijini kwenda kutafuta unafuu wa maisha hali inayowafanya vijana wengi kuishi katika mazingira magumu wawapo mijini kutokana na ukweli kwamba wengi wao hawana ujuzi wa kuwawezesha kuishi mijini kwani sehemu kubwa ya shughuli za mjini zinaitaji mtu awe na ujuzi Fulani ili afanikiwe.
Masanja katika harakati za kilimo |
Hali imekuwa tofauti kwa Msanii na mchekeshaji maarufu wa kipindi chaZe Orijino Comedy, Emmanuel Mgaya maarufu kama Masanja Mkandamizaji ambaye amesema kuwa vijana wanapaswa kufikiria namna ya kuwekeza vijijini hasa kwenye mashamba kwani huko kuna fursa nyingi zenye uwezo wa kuleta mabadiliko katika maisha ya vijana walio wengi ambao wameng’ang’ania mjini na kuendekeza majivuno yasiyo na msingi huko mijini huku maisha yao yakiendelea kudorora siku hadi siku
Akizungumza na mwandishi wetu Masanja Mkandamizaji alisema anafurahi kwani mwaka huu amefanikiwa kuvuna tani kadhaa za zao la mpunga katika shamba lake lililopo Mbarali Estate.
“Nimelimia Mbarali Estate namshkuru Mungu kwa kufanikiwa kuvuna mpunga wangu baada ya kuwekeza shamba lenye ukubwa wa ekari 15, huu ni uwekezaji mzuri unaotoa matunda kwa muda mfupi iwapo utahudumia shamba lako ipasavyo.”
“Vijana wengi wana nguvu na uwezo wa kuingia mashambani ila wanaendekeza ‘usharobaro’ kitu ambacho hakina mavuno kwao,” alisema Masanja aliyetumia mashine ya kisasa katika zoezi hilo.
Aliwaasa vijana kutokukimbia mashambani na badala yake wajiunganishe katika vikundi vya kujikwamua kiuchumi hali itakayowawezesha vijana kupata elimu na uwezo wa kulima kisasa ili wapate mazao mengi nay a kutosha hali itakayowapunguzia vijana walio wengi ugmumu wa maisha.
Masanja ambaye pia ni mwimbaji wa kwaya ya New Jerusalem alisema: “Mimi ni mchungaji mtarajiwa lakini huduma yangu ya uchungaji nimeanzia kwenye kundi langu hili la Ze Komedy, kupitia hilo nina washirika wangu ambao natamani wawe kama mimi mchungaji wao wafuate nyayo zangu, naomba maombi ya watumishi wengine wamuombee Joti,” alisisitiza!
Kwa sasa, Masanja anahudhuria ibada katika kanisa la EAGT, Mito ya Baraka pia amefanikiwa kutoa nyimbo 10 za Injili na tayari album yake ya ‘Hakuna Jipya’ iko mitaani.
No comments:
Post a Comment