(picha si yake)
kwa jina naitwa lisa au mama owen naishi ukerewe
nilibahatika kuolewa
mwaka 1998na nilibahatika kupata watoto wawili wote wa
kiume hivi sasa wa kwanza yupo
kidato cha nne nawa pili ypo darasa la nne.
Baada ya kuolewa na mume wangu tuliweza
kuwa na mafanikio makubwa saana awali tulikuwa tunaishi kwenye nyumba ya familia.ya
mume tulipewa vyumba vitatu kwa kuwa tulikuwa tunaishi na familia yao baada ya miezi
michache tukafanikiwa kujenga nyumba aina ya gorofa moja kwa kupewa msaada mkubwa
saana na.mama yangu mzazi ambaye kwa.sasa ni marehemu baada ya hapo tukahama
kwenye nyumba ya familia.na kuhamia ktk nyumba yetu na maisha yakawa na amani na
furaha mungu akaendelea kutubariki tukanunua viwanja,magari,na mashamba kwa
kusaidiana na mama yangu mzazi baada ya muda maisha yakabadilikaa familia ya
mume.ikawa ndo inampangia maisha mume wangu mie sikuona shida saana mama mkwe'
wangu ndo akawa kila.kitu ktk maisha ya nyumba yetu mara yakaanza manyanyasoo na
vipigoo kwa.saana sasa mwaka.2012 ndio ikawa mwisho wa ndoa yangu kwani alinipiga na
kunifukuza kama mbwa niliondoka na nguo nilizokuwa nimevaa tuu akunipa nafasi hata ya
kuchukua kijiko mbaya zaidi hadi watoto cna uhuru nao watoto ni wanaenda moshi tu
kwa.bibi yao mie cna uhuru nao. ila baada ya kunifukuza nilirudi kwa dadangu na nikapiga
goti na kusali na mungu akajibu maombi yangu na mda wwte wakati npo kwa dadangu
cjawahi kuona ndugu yke yyte hata.kunipigia simu zaidi ya yeye mwanaume kunitumia.sms
za matusi na wakati npo nae hakutaka niajiriwe kokotee kuule kwanj mie nimesomea
mambo ya IT kokote nilipokuwa nikipata kazi anakuja kunidhalilisha saana wakati huo yeye
na utajiri wake cyo wa kununua hata chupi kwangu basi nikawa naishi maisha ya kipigo na
manyanyaso saana baada ya . .mamangu kufariki tukapata mirathi na nilivyokuwa mjinga
hela yoote tukawekeza ktk mitaji ya.maduka tuliyonayo. haikupita mda ndo kanifukuza
nikatoka.
jinsi nilivyoo ikawa bahati kuna nafasi za kazi zilitoka serikalini nika apply hatimae
nikaitwa kwenye interview na nikafanikiwa kufaulu na nikapangiwa kituo cha kazi ktk wilaya
hizi mpya za Dsm nikanza kazi na mungu akaendelea kunigusa na hivi saaa namalizia
nyumba yangu ambayo kwenye hyo site alishakuja na kudai ni kiwanja chake na kuniwekea
x ila mungu ni mwema tuliweza kuyamaliza kisheria! sasa kinachoniuma yeye.hivi sasa
ameshafilisika hana kitu chochote hata.uwezo wa kulipa ada za watoto hana ada zinalipwa
na ndugu zake nikaenda kuomba saaana watoto wangu ili niwapeleke shule familia yao ndo
wasemaji wakuu hawataki kunipa watoto mbaya zaidi watoto kila.kukicha
wanafukuzwa.ada kiasi kwamba watoto wanashuka.kielimu baba yao hana uwezo teena wa
kuwa manage ila wanasema mila za.kichaga mwanamke harusiwi kuondoka na wato to
sasa dada joyce nime
dhulumiwa kiila kituu sasa hata watoto nao sina uhuru nao wanangu bado wadogoo saana
sielewi nifanyaje sina msaada wowote ule na wala.sijui nifanyaje dada joyce.embu nisaidie
sasa hivi ndugu wa mume ndo wananitafuta na kunisii nirudi nikalee watoto na huyo mume
ambae kwa sasa yupo kama amechanganyikiwa kimaisha kwani maduka yoote kafunga
biashara zte hakuna kitu na sasa hivi anatembelea pikipiki magari yoote ameuza pia
viwanja kauza ambavyo vyote hvyo ni jasho langu dada joyce wakati ule mie sina kitu
ndugu zake sikuwaona sasa hivi mungu amenigusa na mie sasa hivi ndo wanataka
nisamehe na kusahau da joyce mie niliteseka saana ktk hyo ndoa vipigo mbele ya watoto
unafukuzwa usiku wa mananee unambiwa kwenda kwenuu huna hadhi ya kulala ktk hili
gorofa wewe ni mbwa tuu cku zinginewe unalala kibarazani hadi kunakuchaa dada sasa
mwaka 2012 ndo nikasema sasa basii acha nikawe bar meid kama alivyokuwa.akiniambia
nikitoka.kwake labda nikawe bar maid nikamwambia sawa.hata hiyo ni kazi bora amani ya
bar maid kuliko maisha haya ninayo ishi. da joyce nimenusurika kuchinjwa watoto wanakuja
kuniokoa natukanwa mbele ya wateja dukani kwani mie ndo nilikuwa muuza duka siku
ingine unapigwa hapo ktk biashara mbele ya wateja aibu dada usipime sasa mda umefika
nataka nikadai changu kwani hadi vitu vya marehemu mamangu niliviacha huko jee na hvyo
navyo sina uhuru wa kuvichukua?
CHANZO: WANAWAKE LIVE
No comments:
Post a Comment