Josephat Torner akiwa kileleni mlima Kilimanjaro
Alizaliwa katika kijiji cha Ngwengwe kilichopo karibu na ziwa Victoria, Mama yake alifariki Josephat alipokuwa na miaka 12.
Tangu mwaka 2012 Josephat amekuwa mpiganiaji wa haki za walemavu wa ngozi Tanzania.
Kupitia chama chake cha Ukerewe Albino sociaty amezunguka mikoa yote Tanzania kuelimisha wananchi juu ya watu wenye ulemavu wa ngozi( albino) Aliyafanya hayo kufuatia mauaji ya Albino yaliyokuwa yakiendelea kwa kasi nchini Tanzania.
Lengo ni kuhakikisha watu wanakuwa na uelewa juu ya albino, na kuachana na imani potovu za kishirikina, Imani ambazo zimesababisha wenye ulemavu wa ngozi Tanzania kuwa vilema na wengi kuuawa kinyama.
Josephat Torner akiwa Kijijini.
Kupitia Filamu yake ya "In the Shadow of under the sun.Josephat alitumia Filamu hiyo kwa kuieleza dunia jinsi walemavu wa ngozi (albino) nchini Tanzania walivyonyimwa haki za kibinadamu pamoja na jinsi wanavyouawa kinyama.
No comments:
Post a Comment