Sunday, 3 January 2016

HOMA YA MANJANO KWA WATOTO MCHANGA:BAADA YA KUZALIWA‏

njano

Manjano yakionekano machoni,paji la uso na puani


Homa ya manjano ni ugonjwa  unawashika watoto wachanga baada ya masaa machache  kuzaliwa .Manjano kawaida huonyesha rangi ya manjano kwenye macho ,paji la uso,nyayo za miguu,kifuani na tumboni ,ukimkagua mtoto vizuri haswa kwenye mwaga wa jua utaona  wanjano kwa urahisi.Homa ya manjano inashika watoto na watu wazima pia.


Dalili za homa ya manjano

Mtoto ataonyesha dalili tofauti ,anaweza akaonyesha zote kwa pamoja au baadhi yake,

: Macho ya mtoto na ngozi kubadili rangi kuwa ya njano

:Homa kali

:Kutapika

:Kulala sana

:Mkojo kuwa brown

Ukiona hizo dalili ni hatari muwaishe hospital.


 manjano

Hali ya mtoto kuwa wanjano kitaalamu inaitwa Jaundice,husababishwa na kemikali inayoitwa bilirubin kuzalishwa kwa wingi  kwenye damu ya mtoto.Bilirubin inapokuwa nyingi  kumletea mtoto madhara . Takwimu inaonyesha watoto wakiume ni rahisi kupata manjano kuliko watoto wa kike,na asilimia 80 ya watoto njiti hupata homa ya manjano wakiwa na siku 5 mpaka 7 baada ya kuzaliwa .


Sababu zinazomfanya mtoto apate manjano Jaundice


1: Mtoto anapokuwa na blood group tofauti na mama  ,anakuwa na hatari ya kupata manjano.

2:Mtoto njiti premature ni rahisi kupata manjano

3:Watoto waliozaliwa na matatizo ya kiafya au infection

4:Mama wenye blood group o wanahatari ya kusababisha mtoto kupata manjano

5: Mama anaepata kisukari kipindi cha mimba )gestational diabetes anaweza zaa mtoto mwenye manjano.

6:Mama kuzalisha maziwa machache kunaweza msababishia mtoto kupata manjano

7:Mtoto mwenye matatizo ya ini nao hupata manjano



 Matatizo ya kiafya anayopata mtoto aliepata manjano
 Mtoto anapopata manjano ni vizuri kutibiwa haraka iwezekanavyo ,lasivyo mtoto atapata haya matatizo

:Kemikali ya bilirubin ikiongezeka sana kwenye damu ya mtoto inaenda adhiri ubongo

: kumsababishia matatizo ya kuto kusikia,

:kuto kuona

:Kushindwa ongea na  kutembea vizuri

:Kifo

:Ulemavu wa kudumu




TIBA

Manjano  hutibika kwa njia tofauti , na huchukua siku 7 mtoto kupona iwapo hatokuwa nayo nyingi mwilini,kama ni nyingi itamchukua zaidi ya siku saba.

1:Maziwa ya mama ni tiba  kubwa, mama anatakiwa kunyonyesha mtoto kwa wingi ili kupunguza kiasi cha billirubin iliozalishwa kwa wingi kwenye damu ya mtoto. Mtoto atolewe nje apigwe na jua , jua linasaidia kupunguza ile sumu.

2: Mtoto,atawekwa kwenye kifaa kiitwacho  Phototheraphy light  kwa masaa 48 au zaidi mpaka daktari atakapo ona sumu imeisha mwilini.



 anapokuwa kwenye phototheraphy  anafunikwa macho ili ule mwanga usimwadhiri macho yake na kuveshwa diaper tu  ili mwanga na hilo joto kuzuia mzunguko wa billrubin kwenye damu ya mtoto.




3:  Njia nyingine ni kubadilishwa damu ila hii atafanyiwa iwapo hali yake inaonyesha ni mbaya zaidi.


NB

Maziwa ya mama ni muhimu sana kwa mtoto hakikisha unamnyonyesha kila baada ya masaa 2 ili kuondoa manjano kwa haraka na kusave maisha ya mtoto,kama maziwa hayatoki hakikisha unamnunulia baby formula )maziwa ya kopo


shukrani kwa Afya ya mama na mtoto.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!