SERIKALI imeendelea kuandaa mazingira ya sehemu itakayotumika kwa ajili ya kumwapisha Rais mteule wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli. Maandalizi ya mazingira hayo yanaenda sambamba na mazoezi ya kijeshi kwa ajili ya gwaride maalumu, litakalofanyika wakati wa kuapishwa kwake katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
HabariLeo lilifanikiwa kutembelea katika uwanja huo na kujionea jinsi mazoezi hayo yanavyoendelea, ambapo mmoja wa askari jeshi aliyekuwa akilinda eneo hilo alisema kinachoendelea ndani ya uwanja huo ni mazoezi ya kijeshi kwa ajili ya siku hiyo.
“Mazoezi ya kijeshi na gwaride yanaendelea humu ndani, kwa sasa wananchi wa kawaida hawaruhusiwi kuingia, ila siku husika ikifika wataruhusiwa,” alisema mwanajeshi huyo. Dk Magufuli anatarajia kuapishwa Novemba 5, mwaka huu baada ya kukamilika kwa taratibu zote za uchaguzi na kukabidhiwa cheti cha ushindi.
No comments:
Post a Comment