Friday, 18 September 2015

Watu wanne wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wa kutumia silaha wameuawa, Arusha.



Watu wanne wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wa kutumia silaha wameuawa usiku wa kuamkia Septemba kumi na saba katika shambulio la kutupiana risasi na askari wa jeshi la polisi wakiwa kwenye harakati za kwenda kufanya tukio la ujambambazi katika duka moja la kubadilisha fedha jijini Arusha.



Akizungumzia tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Leberatus Sabasi anasema askari wake walianza kuwafuatilia watu hao tangu mwezi Agosti baada ya kupata taarifa za kiintelijensia kwamba kuna kundi la majambazi kutoka nchi jirani ya Kenya linalojipanga kuingia nchini kwa lengo la kushirikiana wenzao waliopo mkoani Arusha kwa ajili ya kufanya matukio ya uporaji.
Kwa mujibu wa kamanda Sabasi katika kufuatilia taarifa hizo jeshi hilo lilifanikiwa kumnasa mmoja wao aliyefahamika kwa jina la Sixtus Ngowi ambaye alikiri kushiriki kwenye matukio mbalimbali ya uhalifu na akakubali kutoa ushirikiano wa kuwanasa wenzake na ndipo juzi waliponaswa katika eneo la Chekereni wakiwa wanaelekea kupora kwenye duka la kubadilishia fedha liitwalo Sanya ambapo katika harakati za kurushiana risasi wanne akiwemo yule aliyekua akisaidia polisi walipoteza maisha na wengine wakatoroka.
Baada ya kuuawa watu hao walikutwa na mabegi matatu yaliyokua na bunduki mbili aina ya AK 47, SMG moja, Bastola moja na jumla ya risasi mia kumi na tatu na vitambulisho vitatu vya jamhuri ya Kenya vyenye majina tofauti huku taarifa za kipolisi zikieleza kuwa walengwa wao wakubwa walikua niwafanyabiashara wakubwa wa madini, maduka ya kubadilishia fedha na taasisi za fedha.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!