.jpg)
MWANDISHI WETU
TIMU ya SIMBA YA Dar es Salaam imeanza Ligi Kuu Tanzania Bara kwa ushindi wa bao -1-0 dhidi ya African Sports, katika mchezo uliopchezwa Uwanja wa Mkwakwani, mjini hapa.
Bao hilo la Simba limefungwa katika dakika ya 56 kupitia kwa Hamisi Kiiza baada ya kuunganisha kwa kichwa krosi ya Mussa Hassan ‘Mgosi’.
Na katika michezo mingine iliyochezwa kwenye viwanja tofauti, mabingwa wa Kombe la Kagame, timu ya Azam FC imeifunga Tanzania Prisons mabao 2-1, mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Mabao yalifungwa na Kipre Tchetche katika dakika ya 39 na Farid Mussa katika dakika ya 81 huku la Tanzania Prisons likifungwa dakika ya 60 na Jeremiah Juma.
Katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara, timu ya Ndanda imelazimishwa sare ya bao 1-1 na Mgambo Shooting ya mkoani Tanga.
Katika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, timu ya Toto Africa imeifunga Mwadui ya Shinyanga bao 1-0.
Katika Uwanja wa Sokoine, Mbeya, timu ya Kagera Sugar imeifunga Mbeya City bao 1-0.
Katika Uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma, timu ya Majimaji imeifunga JKT Ruvu bao 1-0.
Katika Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga, timu ya Mtibwa Sugar imeifunga Stand United bao 1-0.













No comments:
Post a Comment