Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimfariji Mke wa Waziri Mkuu, mama Tunu Pinda (kushoto) ambaye alifiwa na Mama yake , Hajjat Pili Mlolwa Rehani, nyumbani kwa marehemu, Tabata Magengeni jijini Dar es salaam Septemba 17, 2015. Kuliani Mama Hasina Kawawa.
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akiwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba Wapili kushoto na Mama Hasina Kawawa waliokwenda kumfariji kufuatia kifo cha Hajjat Pili Mlolwa Rehani,Mama wa Mama Tunu , nyumbani kwa Marehemu, Tabata Magengeni jijini Dar es salaam Septemba 17, 2015.
Makamu wa Rais,Dkt. Mohamed Bilal akimfariji mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda wakati alipokwenda Tabata magengeni jijini Dar es salaam, nyumbani kwa marehemu, Hajjat Pili Mlolwa Rehani ambaye ni mama wa Mama Tunu, aliyefariki Septemba 17, 2015. Kulia ni Mama Hasina Kawawa,watatu kulia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba na wanne kulia ni Naibu Waziri wake Pindi Chana.
Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi akimfariji mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda wakati alipokwenda Tabata magengeni jijini Dar es salaam, nyumbani kwa marehemu, Hajjat Pili Mlolwa Rehani ambaye ni mama wa Mama Tunu, aliyefariki Septemba 17, 2015. Kulia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba na wanne kulia ni Naibu Waziri wake Pindi Chana.Baadhi ya waomboezaji walioshiriki katika mazishi ya Hajjat Pili Mlolwa Rehani, Mama Mzazi wa mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda, nyumbani kwa marehemu jijini Dar es salaam, Septemba 17, 2015.
Makamu wa Rais Mohammed Bilal akishiki kubeba jeneza lenye mwili wa Hajjat Pili Mlolwa Rehani,mama yake Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda katika sala ilitofanyika nyumbani kwa marehemu, Tabata Magengeni jijini Dar es salam Septemba 17,2015.
Waombolezaji wakibeba jeneza lenye mwili wa Hajjat Pili Mlolwa Rehani,Mama wa Mke wa Waziri Mkuu, Tunu Pinda katika mazizi yaliyofanyika kwenye makaburi ya Segerea jijini Dar es slaam Septemba 17, 2015.
No comments:
Post a Comment