Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon amechukua hatua kali kufuatia tuhuma za unyanyasaji wa ngono dhidi ya walinda amani wa umoja wa mataifa huko jamhuri ya afrika ya kati.
Bwana Ban ki -Moon amesema ameomba na kukubali kujiuzulu kwa mjumbe wake wa juu wa jamhuri ya Afrika ya ati , luteni generali Babacar Gaye .
Amesema licha ya kwamba mwanadiplomasia huyo wa muda mrefu kutoka Senegal na afisa wa jeshi ametumikia bila kuchoka kama mjumbe wa umoja wa mataifa , anataka kutuma ujumbe mzito dhidi ya tuhuma hizo.
Anasema anataka kuwa wazi kwamba tatizo hilo limevuka mpaka kwa mjumbe mmoja, au mzozo mmoja, au mtu mmoja.
Unyanyasaji wa ngono ni changamoto ya dunia ambayo inatakiwa kuchukuliwa hatua kali.
Umoja wa mataifa ulituma ujumbe wake unaojulikana kwa kifupi kama MINUSCA mwaka mmoja uliopita.
Tangu hapo kumekuwepo na tuhuma nyingi za unyanysaji wa ngono kwa watoto, kwanza na kikosi cha jumuiya ya kimataifa na baadae walinda amani wa umoja wa mataifa.
Shirika la utetezi wa haki za binadamu lilipeleka ombi katika baraza la usalama la umoja wa mataifa kufanya kipindi maalumu alhamisi kujadili na pia litafanya mkutano kwa njia ya video na wajumbe wake , makanda wa jeshi, na makamishna wa polisi katika operesheni zote za walinda amani ili kusisitiza wajibu wao.
No comments:
Post a Comment