Sunday 2 August 2015

NAOMI ATUPWA JELA MIEZI SITA KWA KUMPIGA PAPARAZI

Naomi-Campbell
Mwanamitindo maarufu duniani, Naomi Campbell.
MWANAMITINDO   maarufu duniani, Naomi Campbell (45) ametupwa jela miezi sita baada ya kukutwa na hatia ya kumpiga paparazi, Gaetano Di Giovanni, Agosti, 2009.


naomi-campbell2
Naomi akiwa katika pozi.
Campbell alidaiwa kumpiga Gaetano Di Giovanni jichoni na mkoba wake baada ya kupigwa picha akiwa na aliyekuwa mchumba wake wakati huo August, 2009.
Mdada huyo ambaye ni mkongwe kwenye masuala ya mitindo, amehukumiwa na Sicilian Court kifungo cha miezi sita jela, Ijumaa ya Julai 31, mwaka huu lakini kifungo chake kinafahamika kama ‘Suspended Prison Term’ ambacho hataingia nyuma ya nondo kwa sasa.

British-model-Naomi-Campbell
‘Suspended Prison Term’ ni kifungo ambacho mshtakiwa haendi jela moja kwa moja baada ya hukumu kutolewa, lakini akivunja sheria katika kipindi hicho (miezi sita) ataenda moja kwa moja jela, na akimaliza muda huo bila kufanya kosa wala kuvunja sheria basi anafutiwa mashitaka.
Hata hivyo, mwanasheria wa Naomi, Guido Carlo Alleva amefungukia kesi hiyo kuwa watakata rufaa.

GPL.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!